-
Iran yamnyonga ajenti wa Mossad aliyekuwa akiifanyia ujasusi Israel
Dec 20, 2025 09:32Idara ya Mahakama ya Iran imetangaza kuwa ajenti wa Shirika la Ujasusi la Israel (Mossad) aliyepatikana na hatia ya kuufanyia ujasusi utawala wa Israel, amenyongwa baada ya kukamilika kwa taratibu zote za kisheria.
-
Rais Pezeshkian atoa mwito wa umoja wa Waislamu duniani
Dec 18, 2025 06:57Rais Masoud Pezeshkian wa Iran amesema Muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu, Imam Rouhullah Khomeini (MA) alikuwa mjumbe wa umoja na mshikamano miongoni mwa watu, akisisitiza kwamba mataifa ya Waislamu yanapaswa yaungane ili maadui wasiweze kuibua mifarakano miongoni mwao.
-
Iran yaalani vikwazo vya upande mmoja vya baharini vya Marekani dhidi ya Venezuela
Dec 18, 2025 04:11Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imetoa taarifa na kulaani vitisho vya Marekani kwamba itaiwekea vikwazo vya baharini Venezuela na kuitaja hatua hiyo kuwa uharamia unaofadhiliwa na serikali.
-
Waziri wa Mambo ya Nje asisitizia tena azma ya Iran ya kutetea haki zake za kisheria za nyuklia
Dec 17, 2025 03:09Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Sayyid Abbas Araghchi amesisitizia azma ya Jamhuri ya Kiislamu ya kutetea haki zake za kisheria za nyuklia kulingana na Mkataba wa Kuzuia Usambazaji wa Silaha za Nyuklia (NPT), akisema sera za nyuklia za Tehran zingali zinaendana na mfumo wa sheria za kimataifa.
-
Iran yaitaka dunia izuie kuendelea mauaji ya Wapalestina Gaza
Dec 16, 2025 03:19Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmail Baghaei, amelaani vikali kuendelea kwa mauaji ya halaiki ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza, akiashiria mashambulizi ya mabomu yanayoendelea kufanywa na Wazayuni na kuzuiwa kwa misaada ya kibinadamu.
-
Mauzo ya chai ya Iran nje ya nchi yaongezeka kwa 48%
Dec 16, 2025 03:12Mkuu wa Shirika la Chai la Iran, Habib Jahansaz amesema mauzo ya chai ya Jamhuri ya Kiislamu nje ya nchi katika miezi minane ya kwanza ya mwaka huu wa kalenda ya Iran (ulioanza Machi 21) yameongezeka kwa asilimia 48, ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.
-
Iran: Madai ya kumiliki visiwa vya Ghuba ya Uajemi ni dhidi ya mamlaka ya kujitawala na ujirani mwema
Dec 15, 2025 23:58Iran imesema kuwa madai yoyote ya kumiliki visiwa vitatu vya Ghuba ya Uajemi yaani Tomb Kubwa, TombNdogo na Bu Musa ni ukiukaji wa kanuni za ujirani mwema na kutoheshimu mamla ya kujitawala ya nchi nyingine.
-
Iran: IAEA haina haki ya kutaka kukagua vituo vilivyoshambuliwa
Dec 15, 2025 08:05Mkuu wa shirika la nyuklia la Iran amekosoa wito wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA wa kufanya ukaguzi mpya kwenye maeneo ya nyuklia yaliyoshambuliwa, akisisitiza kwamba taasisi hiyo ya UN haina itifaki zilizo wazi za kukagua maeneo ambayo yalishambuliwa na utawala wa Israel na Marekani.
-
Pezeshkian: BRICS inatoa fursa ya ushirikiano imara zaidi wa wanachama
Dec 13, 2025 23:23Rais Masoud Pezeshkian wa Iran ameashiria nafasi na uwezo wa kundi la BRICS na kulieleza kama jukwaa muhimu la kuimarisha maingiliano na uhusiano wa kiuchumi na kisiasa miongoni mwa nchi wanachama.
-
Iran yalaani mwenendo wa madola makubwa wa kuitunukia Israel 'haki maalumu' ya kufanyia uchokozi
Dec 12, 2025 07:33Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, sera za mataifa makubwa katika Asia Magharibi zimetengeneza "haki maalumu kwa ajili ya utawala wa Kizayuni," hali ambayo imeiwezesha Israel kufanya uchokozi wa kijeshi katika eneo zima, ikiwa ni pamoja na dhidi ya Iran, bila kukabiliwa na mjibizo wa maana kimataifa kwa uchokozi wake huo.