-
Spika wa Iran: Waislamu wana wajibu wa kukomesha mauaji ya Israel Gaza
Sep 03, 2025 03:43Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) ameyataka mataifa ya Kiislamu kuungana katika vita dhidi ya utawala wa Kizayuni, ambao ameutaja kuwa shetani mkubwa zaidi duniani.
-
Kamanda Mousavi: Jeshi la Iran liko tayari kutoa jibu chungu kwa uchokozi wowote
Sep 03, 2025 03:08Mkuu wa Majeshi ya Iran, Meja Jenerali Abdolrahim Mousavi amesisitiza kuwa vikosi vya ulinzi vya taifa hili viko imara na tayari kutoa jibu madhubuti na chungu kwa uchokozi wowote mpya wa maadui.
-
IRIB yalaani mauaji ya mwanahabari wa Al-Alam huko Gaza
Sep 03, 2025 02:57Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Utangazaji wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB kimelaani vikali mauaji ya Rasmi Jihad Salem, mpigapicha wa kanali yake ya Kiarabu ya Al-Alam, ambaye aliuawa shahidi katika shambulio la Israel huko Gaza jana Jumanne, Septemba 2 alipokuwa akirejea kutoka kazini.
-
Tehran yakadhibisha madai ya nchi za Kiarabu kuhusu visiwa vya Iran na kisima cha gesi cha Arash
Sep 02, 2025 23:05Iran imesisitiza mamlaka iliyonayo kwa visiwa vitatu vilivyoko katika Ghuba ya Uajemi, haki yake kwa kisima cha gesi cha Arash na kuhusu mpango wake wa nyuklia wenye malengo ya amani katika kujibu madai ya uongo katika taarifa ya hivi karibuni ya Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi (GCC).
-
Barua ya pamoja ya Iran, Russia na China yalitaka Baraza la Usalama lipinge kutekelezwa utaratibu wa Snapback
Sep 02, 2025 07:54Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran, China na Russia wameandika barua ya pamoja wakipinga hatua ya nchi tatu za Ulaya ya kuanzisha "utaratibu wa papo kwa hapo au Snapaback " kwa ajili ya kurejesha vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Tehran.
-
Pendekezo la Iran kwa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai; hatua ya kuelekea kwenye mfumo mpya wa dunia
Sep 02, 2025 07:26Katika hotuba yake katika kikao cha Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai, Rais Masoud Pezeshkian wa Iran aliwasilisha utatuzi uliopendekezwa na Iran kwa ajili ya kupanua ushirikiano kati ya wanachama wa jumuiya hiyo kwa lengo la kukabiliana na misimamo ya upande mmoja ya Marekani na Magharibi.
-
Iran, Russia kuimarisha uhusiano wao kupitia mikataba ya muda mrefu
Sep 02, 2025 03:34Rais Masoud Pezeshkian wa Iran, na mwenzake wa Russia, Vladimir Putin wamesisitiza umuhimu wa kutekelezwa Mkataba Kamili wa Ushirikiano wa Kistratejia kati ya nchi mbili hizo.
-
Rais wa Iran azitaka US,EU kukomesha makabiliano, zirejee kwenye diplomasia
Sep 02, 2025 03:12Rais Masoud Pezeshkian wa Iran amesema Marekani na Ulaya zinapasa kuacha mienendo yao kwa msingi wa makabiliano na vitisho, na badala yake zifungamane na diplomasia ili kupata suluhisho lenye "mlingano na haki" kwa suala la nyuklia la Tehran.
-
Rais Pezeshkian ataka kuimarishwa amani na ushirikiano wa kiuchumi katika mkutano wa SCO
Sep 01, 2025 04:31Rais Masoud Pezeshkian ametoa wito kwa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) kuchukua hatua madhubuti na za uwazi ili kuimarisha amani na ushirikiano wa kiuchumi duniani.
-
Pezeshkian: Mkutano wa Shanghai unatoa fursa ya kukabiliana na hatua za upande mmoja za Marekani na Ulaya
Aug 31, 2025 04:02Rais Masoud Pezeshkian wa Iran amesema kuwa mkutano ujao wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) unatoa fursa ya kukabiliana na hatua za upande mmoja za Marekani na Ulaya katika masuala ya kimataifa.