-
Kama si Iran, nani atakayeunusuru ulimwengu na shari ya wazi na iliyojificha ya Israel?
Jan 10, 2025 03:58Kwa miaka mingi sasa Israel imekuwa ikitekeleza sera za ardhi iliyochomwa (scorched-earth policy) katika eneo la Asia Magharibi. Kuanzia mashambulizi yasiyosita katika Ukanda wa Gaza na mauaji ya kimbari ya raia wa Palestina hadi kuwauwa kigaidi wasomi wa nyuklia wa Iran na mashambulizi ya anga dhidi ya Syria, ni sehemu ya sera za Israel ambazo zimejikita katika kueneza vita na hali ya mchafukoge.
-
Mabadilishano ya kibiashara kati ya Iran na Qatar yaongezeka kwa 53%
Jan 09, 2025 07:59Mabadilishano ya kibiashara kati ya Qatar na Jamahuri ya Kiislamu ya Iran yameongezeka kwa kasi katika kipindi cha miezi michache iliyopita.
-
Mifumo mipya ya ulinzi wa anga isiyojulikana kujaribiwa katika mazoezi ya Jeshi la Iran
Jan 07, 2025 03:06Kamanda wa Kambi ya Pamoja ya Ulinzi wa Anga ya Iran ametangaza kuwa vitengo vya ulinzi wa anga vya Jeshi la Taifa na Jeshi la Walinzi wa Mapindizi ya Kiislamu (IRGC) vimewekwa karibu na vituo nyeti, vikiwa na mifumo mipya ya ulinzi wa anga ambayo itafanyiwa mazoezi siku chache zijazo, katika luteka ya Jeshi la Iran
-
Salami: Mhimili wa Muqawama upo katika 'kilele cha nguvu zake"
Jan 06, 2025 10:11Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) amesema kuwa Mhimili wa Muqawama katika eneo la Magharibi mwa Asia upo katika kilele cha nguvu zake.
-
Iran yalaani kuendelea mashambulizi ya Marekani na Uingereza dhidi ya Yemen
Jan 05, 2025 07:58Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani mashambulizi mapya ya anga ya Marekani na Uingereza kwenye miundombinu ya mkoa wa Sa'ada wa kaskazini mwa Yemen.
-
Askofu Mkuu wa Ghana: Taswira ya Iran inaheshimiwa miongoni mwa Wakristo
Jan 05, 2025 04:23John Bonaventure Kwofie, Askofu Mkuu wa Ghana na Kiongozi wa Wakatoliki wa nchi hiyo ameeleza kuwa taswira ya Iran inaheshimiika na kuaminika miongoni mwa waumini wa Kikristo.
-
Rais wa Iran kufanya safari nchini Tajikistan
Jan 05, 2025 00:07Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hivi karibuni anatarajiwa kufanya safari ya kikazi nchini Tajikistan.
-
Araqchi: Tupo tayari kwa mazungumzo yenye tija kuhusu mpango wetu wa nyuklia
Jan 04, 2025 04:00Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa Tehran iko tayari kufanya mazungumzo yenye tija na bila ya kuchelewa kuhusu mpango wake wa nyuklia.
-
Balozi wa Saudia aitwa Wizara ya Mambo ya Nje baada ya Riyadh kuwanyonga raia 6 wa Iran
Jan 02, 2025 04:17Mkurugenzi Mkuu wa Masuala ya Kibalozi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema: Balozi wa Saudi Arabia mjini Tehran ameitwa wizarani hapo na kukabidhiwa malalamiko ya kimmandishi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa hatua ya Saudia ya kuwanyonga raia sita wa Iran waliokuwa wamefungwa jela nchini humo, hatua ambayo imeelezwa kuwa inapingana na mwenendo wa mashirikiano ya vyombo vya mahakama yaliyopo baina ya nchi mbili.
-
Gharib Abadi: Iran ni mhanga na iko mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya ugaidi
Jan 01, 2025 09:10Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran anayehusika na masuala ya kisheria na kimataifa amesema kuwa ugaidi ni tatizo linalotishia amani na utulivu wa jamii na kwamba Iran ni mhanga wa uovu huu, na daima iko mstari wa mbele katika vita dhidi ya ugaidi.