-
Safari ya Waziri Mkuu wa Iraq Tehran wakati wa mgogoro wa Gaza
Nov 07, 2023 07:46Waziri Mkuu wa Iraq Mohammad Shia al-Sudani, jana asubuhi akiwa ziarani hapa mjini Tehran alikutana na kufanya mazungumzo na Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
-
Wanamuqawama wa Iraq washambulia kambi nne za Marekani huko Iraq na Syria
Nov 06, 2023 07:05Kwa mara ya nne leo asubuhi wanamuqawama wa Iraq wameshmbulia kambi za jeshi la Marekani huko Iraq na Syria.
-
Kata'ib Hizbullah: Ziara ya Blinken nchini Iraq haikubaliki
Nov 06, 2023 03:00Harakati ya Muqawama ya Kata'ib Hizbullah ya Iraq imetishia kushadidisha hali ya taharuki iwapo Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Anthony Blinken atafanya safari ya kuitembelea Baghdad.
-
Kambi za kijeshi za Marekani zashambuliwa kwa droni Iraq, Syria
Nov 04, 2023 03:03Vituo viwili vya kijeshi vya Marekani vimeshambuliwa katika hujuma za ndege zisizo na rubani (droni) katika eneo la Kurdistan la kaskazini mwa Iraq na katika mkoa wa Hasaka, mashariki mwa Syria.
-
Wanamuqawama wa Iraq waishambulia kwa droni kambi ya Marekani ya Ain al Asad
Oct 27, 2023 14:09Kundi jina la Mujahidina wa Muqawama wa Kiislamu wa Iraq wameshambulia kwa ndege isiyo na rubani (droni) mahali walipo vikosi vamizi vya Marekani katika kambi ya Ain al Asad huko Iraq.
-
Vladimir Putin: Wakati umefika wa kutangazwa nchi huru ya Palestina
Oct 11, 2023 02:57Rais Vladimir Putin wa Russia amezungumzia kushindwa siasa za kibeberu za rais wa Marekani, Joe Biden za kuingilia masuala ya eneo la Asia Magharibi na kutilia mkazo wajibu wa kutekelezwa maamizio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa yanayosisitizia kuundwa nchi huru ya Palestina.
-
Ayatullah Sistani: Waislamu wote wana wajibu wa kuwasaidia Wapalestina
Oct 10, 2023 14:09Kiongozi wa juu wa kidini wa Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Iraq ametoa mwito kwa Waislamu kote duniani kuwaunga mkono, kuwahami na kuwasaidia wananchi wa Palestina, wakati huu ambapo utawala wa Kizayuni wa Israel unaendelea kufanya mashambulizi ya kikatili dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Gaza.
-
Ajuza wa Kiiraq aliyeishi umri mrefu zaidi afariki dunia akiwa na umri wa miaka 138
Oct 05, 2023 13:38Mwanamke mzee zaidi nchini Iraq ameaga dunia katika eneo la al-Islah, lililoko mashariki mwa mji wa Nasiriyah akiwa umri wa miaka 138.
-
Al Sudani: Iraq inapinga kukiukwa mamlaka ya kujitawala ya nchi jirani
Oct 04, 2023 06:48Waziri Mkuu wa Iraq amesisitiza kwa mara nyingine tena kwamba nchi yake haitageuzwa kuwa sehemu ya kukika mamlaka ya kujitawala ya nchi yoyote ile hasa nchi jirani.
-
Kamanda wa jeshi la Iraq: Hatuhitaji wanajeshi wa kigeni wawepo nchini
Sep 28, 2023 14:17Kamanda wa operesheni za pamoja za vikosi vya ulinzi vya Iraq amesema: "nchi hii ina uwezo unaohitajika wa kupambana na magaidi na wala haihitaji kuwepo askari wa kigeni".