Wanamuqawama wa Iraq washambulia kambi nne za Marekani huko Iraq na Syria
(last modified Mon, 06 Nov 2023 07:05:43 GMT )
Nov 06, 2023 07:05 UTC
  • Wanamuqawama wa Iraq washambulia kambi nne za Marekani  huko Iraq na Syria

Kwa mara ya nne leo asubuhi wanamuqawama wa Iraq wameshmbulia kambi za jeshi la Marekani huko Iraq na Syria.

Chanzo cha habari kimeripoti juu ya  shambulio la ndege isiyo na rubani kwenye kambi kubwa zaidi ya Marekani katika eneo la al-Tanf nchini Syria na kambi ya Ain al-Asad kama kambi kubwa zaidi ya Marekani nchini Iraq. 

Ripoti hiyo imeeleza kuwa, muqawama wa Kiislamu wa Iraq leo asubuhi umeshambulia kwa droni makao ya vikosi vamizi vya Marekani kandokando ya uwanja wa ndege wa Arbil nchini humo. Wakati huo huo vyombo vya habari vimetangaza kuwa kambi mbili za wanajeshi vamizi wa Marekani zimeshambuliwa katika mkoa wa al Anbar na huko Baghdad mji mkuu wa Iraq. 

Mashambulizi haya dhidi ya kambi ya vikosi vamizi vya Marekani yametekelezwa baada ya mazungumzo ya masaa kadhaa ya Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani na Waziri Mkuu wa Iraq Muhammad Shia al Sudani huko Baghdad. Katika mazungumzo hayo, Blinken ametoa wito wa kutoshambuliwa kambi na wanajeshi wa Marekani katika eneo.  

Awali Harakati ya Kataeb Hizbullah ya Iraq ilitahadharisha vikali kuhusu safari ya Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani huko Iraq. Katika siku za karibuni pia kambi za kijeshi za Marekani zimehambuliwa mara kadhaa na ndege zisizo na rubani na roketi huko Iraq na Syria.  

Tags