-
Mawaziri 13 wa Mambo ya Nje wakiwemo 6 wa G7 waitaka Israel isitishe uvamizi wa ardhini wa Rafah
May 17, 2024 04:46Shirika la habari la DPA la Ujerumani limeripoti kuwa mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi 13 wametia saini barua ya kuuonya na kuutaka utawala wa Kizayuni wa Israel usitishe uvamizi wake wa ardhini katika eneo la Rafah kusini mwa Ukanda wa Ghaza na kuruhusu misaada zaidi kuwafikia Wapalestina.
-
HAMAS: Mashambulio ya Israel yameua 70% ya mateka wa Kizayuni
May 17, 2024 04:43Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imesema mashambulizi ya utawala ghasibu wa Israel katika Ukanda wa Ghaza, unaokabiliwa na vita vya mauaji ya kimbari ya utawala huo ghasibu, yameua asilimia 70 ya mateka wa Kizayuni, ambao wanashikiliwa na harakati hiyo ya muqawama tangu ilipotekelezwa operesheni ya mwezi Oktoba ya Kimbunga cha Al-Aqsa.
-
Italia yaitaka Israel isitishe operesheni za kijeshi Rafah
May 17, 2024 03:40Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia ameutaka utawala wa Kizayuni wa Israel ukomesha operesheni zake za kijeshi katika mji wa Rafah, wa kusini mwa Ukanda wa Gaza.
-
AFC yataka FIFA iifutie uanachama Israel kutokana na jinai zake Gaza
May 16, 2024 08:51Shirikisho la Soka Asia (AFC) limetangaza kuunga mkono ombi la Palestina la kulitaka Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) liifutie uanachama Israel katika taasisi hiyo kubwa zaidi ya kandanda duniani, kutokana na utawala huo wa Kizayuni kutenda jinai kubwa dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.
-
UK, Ufaransa na Ujerumani zaonywa kwa kutuma ndege kuilinda Israel katika Operesheni ya Ahadi ya Kweli
May 16, 2024 03:55Brigedia Jenerali Esmail Qa’ani, Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ametoa onyo kwa Uingereza, Ujerumani na Ufaransa baada ya nchi hizo tatu za Troika ya Ulaya kupeleka ndege zao za kivita kuulinda utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya operesheni ya kulipiza kisasi ya Ahadi ya Kweli iliyofanywa na Iran mwezi uliopita wa Aprili.
-
Marekani kukanusha tena kutokea mauaji ya kimbari huko Ukanda wa Gaza, ni kukana ukweli ulio wazi
May 16, 2024 00:55Licha ya Wapalestina zaidi ya elfu 35,000 kuuawa shahidi na utawala wa kigaidi wa Israel huko Ukanda wa Gaza, lakini Jake Sullivan, Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Ikulu ya White House nchini Marekani amedai bila kuona haya kwamba serikali ya Rais Joe Biden haiyachukulii mauaji hayo kuwa ni mauaji ya halaiki.
-
"Mauaji ya watoto 15,000 wa Gaza yanaashiria mwisho wa Israel"
May 14, 2024 23:49Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema hakuna shaka kuwa mauaji ya watoto zaidi ya 15,000 wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza itakuwa chachu ya kuharakisha mchakato wa kuporomoka na kusambaratika utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Iran: Israel ni nembo ya ugaidi ulioratibiwa duniani
May 14, 2024 08:27Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imeutaja utawala wa Kizayuni wa Israel kama nembo kuu ya ugaidi ulioratibiwa duniani.
-
Makumi ya Wapalestina wauawa katika hujuma za Israel Gaza
May 14, 2024 07:35Ndege za kivita za utawala wa Kizayuni wa Israel zimefanya mashambulizi mapya ya anga dhidi ya maeneo tofauti ya Ukanda wa Gaza na kuua shahidi makumi ya Wapalestina, wakiwemo watoto wadogo na wanawake.
-
Uingereza yatupilia mbali miito ya kuitaka isitishe uuzaji silaha kwa Israel
May 13, 2024 00:35Serikali ya Uingereza imekataa miito ya kuitaka ifuate mwelekeo ulioonyeshwa na Marekani wa kutishia kusitisha baadhi ya mauzo ya silaha kwa utawala wa Kizayuni wa Israel ikiwa utafanya operesheni kubwa ya ardhini katika mji wa Rafah kusini mwa Ukanda wa Ghaza unaowapa hifadhi wakimbizi Wapalestina wapatao milioni moja na laki nne.