May 17, 2024 07:10 UTC
  • Italia yaitaka Israel isitishe operesheni za kijeshi Rafah

Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia ameutaka utawala wa Kizayuni wa Israel ukomesha operesheni zake za kijeshi katika mji wa Rafah, wa kusini mwa Ukanda wa Gaza.

Antonio Tajani ametoa mwito huo katika mazungumzo yake ya simu na Israel Katz, Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel na kuongeza kuwa, kuna haja ya kusitishwa mapigano katika Ukanda wa Gaza.

"Serikali ya Italia inatoa mwito kwa Israel kukomesha operesheni za kijeshi Rafah. HAMAS inapasa kuwaachia huru mara moja mateka, na pia kuna haja ya usitishaji vita na kuruhusu misaada ya kibinadamu kuingia Gaza," ameongeza Tajani.

Mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu wa Italia ameeleza bayana kuwa, kunapaswa kuchukuliwa hatua za kuzuia kuwa mbaya zaidi hali hatarishi na tete katika eneo la Asia Magharibi. 

Amesema suala la hali ya haki za binadamu hii leo lina umuhimu mkubwa kwa ajili ya kudhamini amani ikiwa moja ya dharura katika medani ya kimataifa, na kupatiwa haki za kimsingi wananchi wa Palestina.

Maandamano ya kuwaunga mkono Wapalestina mjini Rome

Mara kwa mara, wananchi wa Italia na Wapalestina wanaoishi katika nchi hiyo ya Ulaya wamekuwa wakiandamana na kulaani vikali jinai za utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Waandamanaji hao wamekuwa wakitoa wito wa kukomeshwa jinai za Israel dhidi ya Wapalestina na kutaka wananchi hao kupatiwa haki zao zote zilizoporwa na maghasibu wa Kizayuni.

Tags