HAMAS: Mashambulio ya Israel yameua 70% ya mateka wa Kizayuni
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i111854-hamas_mashambulio_ya_israel_yameua_70_ya_mateka_wa_kizayuni
Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imesema mashambulizi ya utawala ghasibu wa Israel katika Ukanda wa Ghaza, unaokabiliwa na vita vya mauaji ya kimbari ya utawala huo ghasibu, yameua asilimia 70 ya mateka wa Kizayuni, ambao wanashikiliwa na harakati hiyo ya muqawama tangu ilipotekelezwa operesheni ya mwezi Oktoba ya Kimbunga cha Al-Aqsa.
(last modified 2026-03-03T12:46:59+00:00 )
May 17, 2024 04:43 UTC
  • HAMAS: Mashambulio ya Israel yameua 70% ya mateka wa Kizayuni

Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imesema mashambulizi ya utawala ghasibu wa Israel katika Ukanda wa Ghaza, unaokabiliwa na vita vya mauaji ya kimbari ya utawala huo ghasibu, yameua asilimia 70 ya mateka wa Kizayuni, ambao wanashikiliwa na harakati hiyo ya muqawama tangu ilipotekelezwa operesheni ya mwezi Oktoba ya Kimbunga cha Al-Aqsa.

Khalil al-Hayya, Naibu Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas, ametangaza habari hiyo katika mahojiano na mtandao wa televisheni wa al-Manar wa Lebanon na kuongeza kuwa adui mzayuni anataka kuwaokoa mateka waliosalia kwa nguvu, na matokeo yake ni kuwaua kwa kuwashambulia kwa mabomu.

Watu wapatao 250 walichukuliwa mateka tarehe 7 Oktoba mwaka jana wakati wa operesheni ya kulipiza kisasi ya Kimbunga cha Al-Aqsa iliyotekelezwa na makundi ya mapambano na Muqawama ya Ghaza.

Hamas iliwaachilia huru mateka 105 wakati wa mapatano ya kusitisha mapigano kwa muda wa wiki moja yaliyofikiwa mwishoni mwa Novemba.

Hivi majuzi, harakati hiyo ya Muqawama ya Palestina ilikubali pendekezo lingine la mapatano ya kuwezesha kusitishwa uvamizi na jinai za Israel dhidi ya Ghaza na kuachiliwa huru mateka wengine, hata hivyo utawala huo wa Kizayuni ulikataa pendekezo hilo lililosimamiwa na Marekani, Qatar na Misri.

Katika sehemu nyingine ya mahojiano hayo, Al-Hayya ametilia mkazo tena matakwa ya Hamas akisema makubaliano yoyote ya usuluhishi yatakayofikiwa inapasa yaamuru kusitishwa kamili na katika pande zote uchokozi wa Israel, kuondoka vikosi vyote vya utawala huo huko Ghaza, na kisha ndipo yatekelezwe makubaliano ya kubadilishana mateka.

Afisa huyo wa Hamas ameashiria pia kushindwa kwa utawala wa Israel kufikia malengo yake ya vita, ikiwa ni pamoja na kuusambaratisha Muqawama na kusema: "baada ya miezi minane ya uchokozi na uvamizi, adui ameshindwa kuufuta Muqawama huko Ghaza licha ya vitendo vyote vya kivamizi"…/