Jan 09, 2017 16:22
Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ametoa ujumbe wa rambirambi kwa niaba ya Serikali na wananchi wa Afrika Kusini kufuatia kifo cha Ayatullah Hashemi Rafsanjani, Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Iran na Spika Mstaafu wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran).