Sep 14, 2016 03:25 UTC
  • Zuma alalamikia kutusiwa na vyama vya upinzani bungeni

Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini amelalamikia kitendo cha vyama vya upinzani nchini humo cha kumtusi mara anapokuwa akihutubia bungeni na kumtaka Spika wa Bunge achukue hatua kukomesha jambo hilo.

Akihutubia bungeni, Rais Jacob Zuma amesema kuwa kila anapokuja bungeni hukabiliwa kwa maneno makali na kutusiwa na wabunge. Amesema badala ya yeye kujibu maswali anaketi bungeni na kutusiwa kwa maneno kama mtenda jinai, mwizi n.k. Amesema anadhani bunge la Afrika kusini linapaswa kuchukua hatua katika uwanja huo.  

Rais Zuma akiwaangalia wabunge wa upinzani wanaomshambulia kwa maneno makali 

Itakumbukwa kuwa Rais Zuma amekuwa akikabiliwa na kashfa ya ufisadi wa fedha ambapo mwezi Machi mwaka huu Mahakama ya Katiba ya Afrika Kusini ilimuamuru arejeshe dola milioni 16 fedha za umma alizotumia kukarabati nyumba yake ya kifahari; hatua iliyozusha makelele na malalamiko ya vyama vya upinzani vilivyosema kwamba Zuma anapasa kujiuzulu kutokana na kashfa hiyo. Rais Jacob Zuma kwa upande wake alikanusha tuhuma hizo za kufuja fedha za umma.

 

Tags