Nov 01, 2016 02:47 UTC
  • Ban Ki-moon aiomba Afrika Kusini isijiondoe ICC

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amempigia simu Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini na kumsihi afute uamuzi wa nchi hiyo kujiondoa ICC.

Katika mazungumzo hayo, Ban amemshukuru Zuma kwa mchango wake katika masuala ya amani Afrika na suala la mabadiliko ya tabianchi.

Vile vile amemueleza Rais Zuma kuwa amesikitishwa sana na uamuzi wa nchi hiyo wa kujitoa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu,ICC, na ameisihi nchi hiyo kuendelea na juhudi zake katika masuala ya haki na uwajibikaji, na kwamba ni matumaini yake kuwa nchi hiyo itazingatia uamuzi wake kabla haujatekelezwa miezi kumi na mbili ijayo.

Ban pia ameiomba nchi hiyo kutoa wito kwa serikali ya Sudan Kusini kukomesha uhasama na kurudi katika mchakato jumuishi wa kisiasa. Nchi kadhaa za Kiafrika zimetishia kujiondoa kwenye mahakama hiyo kutokana na hatua yake ya kuendelea kuwasakama viongozi wa nchi za bara hilo, huku ikifumbia macho jinai zinazofanywa na viongozi wa Magharibi.

Ban ki Moon

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC amesema licha ya kuwa mahakama hiyo imepata pigo kufuatia hatua ya nchi tatu za Afrika kuanzisha mchakato wa kujiondoa kwenye Mkataba wa Roma, lakini hatua hiyo haiwezi kuzuia wala kutatiza shughuli za kila siku za mahakama hiyo.

Tags