-
Radiamali ya Ulaya kuhusiana na stratijia mpya ya Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
May 23, 2018 23:38Federica Mogherini, Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya ametoa radiamali yake kupitia tovuti rasmi ya umoja huo kufuatia stratijia mpya iliyotangazwa na Mike Pompeo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani dhidi ya Iran, akitangaza kufungamana kikimilifu EU na makubaliano ya nyuklia ya Iran maaruku kwa jina la JCPOA.
-
Matamshi yaliyo dhidi ya Iran ya Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani
May 21, 2018 23:35Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani amekariri madai yaliyo dhidi ya Iran na kwa mara nyingine tena kuituhumu Tehran kuwa inasababisha ukosefu wa amani katika eneo.
-
Qassemi: Nchi za Ulaya zitoe dhamana kuwa maslahi ya Iran yatazingatiwa katika mapatano ya JCPOA
May 21, 2018 08:47Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema: "Katika muda mfupi uliosalia, nchi za Ulaya zinapaswa kutoa dhamana kuwa maslahi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yatalindwa baada ya Marekani kujiondoa katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA."
-
Iran haitafanya mazungumzo kuhusu maudhui yoyote isipokuwa Mapatano ya Nyuklia ya JCPOA
May 21, 2018 07:51Karibu wiki mbili baada ya Marekani kujiondoa katika mapatano ya nyuklia ya Iran yanayojulikana kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekeelzwaji, JCPOA, kumefanyika mazungumzo mjini Brussels baina ya wakuu wa Iran na Umoja wa Ulaya.
-
Zarif: EU ichukue hatua za kivitendo katika kuendeleza ushirikiano na Iran
May 20, 2018 22:02Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema: "Umoja wa Ulaya unapaswa kuchukua hatua za kivitendo na kuongeza uwekezaji wake nchini Iran katika kuendeleza ushirikiano wa kibiashara na Tehran."
-
Velayati: Dhamana imara ichukuliwe kutoka nchi za Ulaya kuhusu mapatano ya nyuklia
May 20, 2018 10:18Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya kimataifa amesema: "Mtazamo wa Jamhuri ya Kiislamu ni kuwa, katika mazungumzo na nchi za Ulaya kunapaswa kupatikane dhamana imara ili mapatano ya nyuklia ya JCPOA yasivurugike."
-
Taarifa ya Troika ya Ulaya yaunga mkono kulindwa makubaliano ya JCPOA
May 17, 2018 09:59Wakuu wa Ufaransa, Ujerumani na Uingreza baada ya kufanya kikao chao cha pande tatu katika mji mkuu wa Bulgaria, Sophia kwa mara nyingine tena wametaka kulindwa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA kwa hali zote.
-
Russia na Ufaransa kuendelea kufungamana na JCPOA
May 15, 2018 22:11Siku chache baada ya Rais Donald Trump kutangaza kuiondoa Marekani katika makubaliano ya nyuklia ya Iran yanayofahamika kama JCPOA, kwa mara nyingine tena marais wa Russia na Ufaransa wamesisitizia umuhimu wa pande zilizosalia kuendelea kufungamana na mapatano hayo ya kimataifa.
-
Zarif aanza safari ya kuzitembelea China, Russia na Brussels kuhusu JCPOA
May 13, 2018 03:02Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo Jumapili ameelekea mjini Beijing, katika safari ya kuzitembelea China, Russia na Ubelgiji; ziara yenye lengo la kutathmini utayarifu wa jamii ya kimataifa wa kuihakikishia Iran kuwa itasalia katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, licha ya Marekani kujiondoa kwenye mapatao hayo.
-
Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje US waacha kazi baada ya hatua ya Trump kujiondoa JCPOA
May 12, 2018 09:23Gazeti la Foreign Policy la nchini Marekani, limefichua wimbi la kuacha kazi kwa maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, baada ya hatua ya Rais Donald Trump ya kuiondoa nchi hiyo katika makubaliano ya nyuklia ya Iran JCPOA.