-
Dakta Salehi: Jibu la Iran kwa ukiukaji wa makubaliano ya JCPOA litakuwa la kushtukiza
Aug 10, 2017 09:28Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran (AEOI) amesema kuwa, kama Iran ikitaka kutoa jibu kwa ukiukaji wa makubaliano ya nyuklia yanayojulikana kama Mpango Kamili wa Utekelezaji wa Pamoja (JCPOA) basi jibu lake litakuwa ni la kushtukiza.
-
Iran: US ijiandae kwa matokeo mabaya ikikiuka JCPOA
Aug 09, 2017 03:08Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameitahadharisha Marekani na matokeo mabaya itakayoyapata iwapo itaamua kukiuka makubaliano ya nyuklia ya Vienna.
-
Araqchi: Vikwazo vipya vya US vinalenga kuisambaratisha JCPOA
Aug 03, 2017 02:55Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema hatua ya Rais Donald Trump wa Marekani kusaini sheria ya vikwazo vipya dhidi ya Tehran ni njama ya Washington ya kutaka kusambaratisha makubaliano ya nyuklia ya Vienna yanayojulikana kwa kifupi kama JCPOA.
-
Iran: Yaishitaki Marekani kwa hatua yake ya kuiwekea vikwazo vipya Tehran
Aug 01, 2017 09:44Spika wa Majilisi ya Ushauri ya Kiislamu yaani Bunge la Iran sambamba na kubainisha kwamba, ukiukaji wa makubaliano ya nyuklia yanayojulikana kwa kifupi kama JCPOA uliofanywa na Marekani uko wazi, amesema kuwa Jamhuri ya Kiislam ya Iran imewasilisha mashitaka kwenda kwa baraza na kamisheni inayosimamia makubaliano hayo, kutokana na hatua ya Washington ya kuliwekea taifa hili vikwazo vipya.
-
Araqchi: Hatua ya Kongresi ya Marekani ni mwendelezo wa uadui wa Washington dhidi ya Iran
Jul 30, 2017 03:26Mkuu wa timu ya Iran ya kufuatilia utekelezwaji wa makubaliano ya nyuklia yanayojulikana kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) amesema kuwa, hatua ya hivi karibuni ya Kongresi ya Marekani ya kupasisha vikwazo vipya dhidi ya Iran ni hatua ya kiuadui na chuki dhidi ya Tehran.
-
Kamisheni ya Bunge la Iran yapasisha mambo jumla ya kukabiliana na chokochoko za Marekani
Jul 29, 2017 08:59Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Siasa za Kigeni katika Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imepasisha katika kikao chache cha dharura hii leo, mambo jumla ya kukabiliana na hatua za kiuhasama na kiuadui za Marekani dhidi ya taifa hili.
-
New York Times: Trump anafanya njama za kuionyesha Iran kuwa ndio iliyokiuka JCPOA
Jul 28, 2017 21:52Mchambuzi wa masuala ya kisiasa na mhariri wa gazeti la The New York Times amesema kuwa, Rais Donald Trump wa Marekani, anafanya njama za kuionyesha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa ndiyo iliyokiuka makubaliano ya nyuklia yanayojulikana kwa kifupi kama JCPOA.
-
Boroujerdi: Marekani inapasa kuheshimu makubaliano ya kimataifa
Jul 27, 2017 03:19Mkuu wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amesema kuwa Marekani inapasa kujifunza maadili ya kisiasa kuhusu makubaliano ya kimataifa na kuheshimu makubaliano hayo.
-
Russia: Makubaliano ya JCPOA yamefichua jinsi Marekani inavyokiuka sheria za kimataifa
Jul 22, 2017 12:20Mkuu wa Kituo cha Stratijia za Kisiasa nchini Russia, Sergei Mikheev amesema kuwa, kitendo cha Marekani kukiuka makubaliano ya nyuklia yanayojulikana kwa kifupi kama JCPOA, kimeidhihirisha nchini hiyo kwamba ni mkiukaji mkubwa wa sheria na mikataba ya kimataifa duniani.
-
Russia yalaani hatua ya Marekani ya kuiwekea vikwazo vipya Iran
Jul 21, 2017 03:14Mkuu wa Idara ya Kuzuia na Kudhibiti Silaha iliyo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia, Mikhail Ulyanov amelaani hatua ya kiuhasama ya Marekani katika kuiwekea Jamhuri ya Kiislamu ya Iran vikwazo vipya na kusema kuwa, vikwazo hivyo havijazingatia sheria zozote zile.