Abubakar al Baghdadi kiongozi wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh ametoa amri ya kunyongwa magaidi 320 walio chini ya usimamizi wake kwa tuhuma za kufanya usaliti na kupelekea kupata kipigo kikali kundi hilo la kigaidi huko Iraq na Syria.
Kituo kiitwacho Uangalizi wa Haki za Binadamu nchini Syria kimeripoti kuwa kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh limeua kwa kuwanyonga watu zaidi ya elfu tano nchini humo.
Kufuatia kutolewa hukumu ya kifo dhidi ya vijana sita wa Bahrain na mahakamu ya kijeshi ya Aal Khalifa, Wabahrain wameandamana katika pembe tofauti za nchi hiyo ndogo ya Ghuba ya Uajemi kulalamikia ukandamizaji wa utawala huo dhidi yao.
Mahkama ya rufaa ya kijeshi nchini Bahrain, imetoa hukumu ya adhabu ya kifo dhidi ya raia sita wa nchi hiyo kwa tuhuma bandia kwamba walijaribu kupanga shambulizi dhidi ya kamanda wa vikosi vya ulinzi nchini humo.
Baraza la uongozi la serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya imesema kuwa inawajibika kuwafuatilia kisheria wale wote waliohusika na mauaji ya hadharani nchini humo.
Waziri wa Mawasiliano wa Utawala Haramu wa Israel, Ayoob Kara ametishia kuwanyonga waandishi wa habari na wamiliki wa vyombo hivyo ndani ya utawala huo.
Jumuiya ya Demokrasia na Haki za Binadamu ya Bahrain (ADHRB) imetangaza kuwa, hukumu za vifo dhidi ya wapinzani zimeongezeka sana katika nchi tatu za Saudi Arabia, Bahrain na Kuwait.
Kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh limemuua mmoja wa makamanda wake wa ngazi ya juu baada ya kutaka kujisalimisha kwa askari wa Kikurdi wa Peshmerga.
Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limeitaka Saudi Arabia itupilie mbali uamuzi wa kuwanyonga wapinzani 14 wa serikali ya nchi hiyo waliolazimishwa kukiri makosa ambayo hawajafanya kutokana na mateso na manyanyaso.
Mahakama za Saudi Arabia imewahukumu kifo Waislamu 29 wa madhehebu ya Shia nchini humo.