Oct 11, 2018 08:08 UTC
  • Al Baghdadi aamuru kunyongwa mamia ya magaidi wa Daesh

Abubakar al Baghdadi kiongozi wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh ametoa amri ya kunyongwa magaidi 320 walio chini ya usimamizi wake kwa tuhuma za kufanya usaliti na kupelekea kupata kipigo kikali kundi hilo la kigaidi huko Iraq na Syria.

Duru za habari zimearifu kuwa amri hiyo ya kunyongwa imeanza kutekelezwa, na makamanda wa ngazi ya juu wa Daesh wakiwemo Abu al Bara al Ansari, Saifuddin al Iraqi, Abu Ayman al Muwahid, Abu Qassim al Halabi na Marwan Hadidi al Suri ni miongoni mwa makamanda watakaonyongwa.  

Amri hiyo ya kunyongwa mamia ya magaidi wa kundi la Daesh imepelekea kutoroka wanachama wengi wa kundi hilo la kigaidi na kitakfiri. Imeelezwa kuwa kiongozi wa Daesh siku chache zijazo atatoa orodha nyingine yenye majina ya wanachama wake watakaonyongwa. Kabla ya kutekelezwa amri hii ya kunyongwa, mwezi Septemba mwaka huu pia kundi la kigaidi la Daesh liliwanyonga wanachama wake kadhaa katika mkoa wa Diyala mashariki mwa Iraq kwa kukataa kutekeleza oparesheni ya kujilipua kwa mabomu. 

Daesh ikiwauwa wanachama wake huko Iraq 

 

Tags