Jan 14, 2018 04:41 UTC
  • Israel yatishia kuwanyonga waandishi wa habari

Waziri wa Mawasiliano wa Utawala Haramu wa Israel, Ayoob Kara ametishia kuwanyonga waandishi wa habari na wamiliki wa vyombo hivyo ndani ya utawala huo.

Kara ametoa vitisho hivyo katika kongamano la kila mwaka la chama chake mjini Eilat, kusini mwa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) na kusisitiza kwamba, kunaandaliwa sheria muhimu kuhusiana na vyombo vya habari. Ameongeza kwa kusema kuwa, kutekelezwa kwa sheria hizo mpya kutasaidia kudhibiti zaidi vyombo vya habari na chombo kitakachokiuka sheria hizo kitakabiliwa na adhabu kali ikiwemo kunyongwa muhusika wake. 

Mmoja wa waandishi wa habari Israel akiwa chini ya ulinzi

Oren Hassan, mmoja wa wawakilishi katika bunge la utawala huo khabithi wa Israel (Knesset) ameeleza kukerwa na matamshi hayo ya Waziri wa Mawasiliano wa Utawala Haramu wa Israel. Kabla ya hapo pia Israel iliwafutia vibali vya kazi waandishi kadhaa wa habari baada ya waandishi hao kufichua jinai zilizofanywa na askari wa utawala huo maarufu kwa kutenda jinai dhidi ya binadamu.

Tags