Sep 06, 2017 03:54 UTC
  • Viongozi wa Daesh waendelea kujisalimisha kwa askari wa Iraq, wengine wauawa

Kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh limemuua mmoja wa makamanda wake wa ngazi ya juu baada ya kutaka kujisalimisha kwa askari wa Kikurdi wa Peshmerga.

Televisheni ya Iraq ya al-Sumaria News imeripoti kuwa, wanachama wa kundi hilo la kigaidi wamemuua Ibrahim al-Aziz, mmoja wa makanda wa ngazi za juu katika kijiji cha al-Khan, wakati alipokuwa akijaribu kujisalimisha kwa askari hao wa Kikurdi katika mji wa Kirkuk, Iraq.

Baadhi ya viongozi wa genge la kigaidi la Daesh

Kwa mujibu wa habari, akthari ya makamanda wa kundi hilo la Daesh (ISIS) akiwemo Mahmud Khamis al-Fadhlawi, Mkuu wa Polisi wa Daesh na Muhammad Idan al-Isafi, Msimamizi wa Fedha wa kundi hilo, wamejisalimisha kwa askari wa Kikurdi wa Peshmerga katika mji wa al-Hawija. Inafaa kuashiria kuwa, baada ya kukombolewa mji wa kistratijia wa Tal-Afar, magharibi mwa mkoa wa Nainawa (Nineveh) kaskazini mwa Iraq kutoka kwa wanachama wa kundi la Daesh, askari wa Iraq kwa kushirikiana na harakati ya wananchi ya Hashdu sh-Sha'abi wanajiandaa kuukomboa mji wa al-Hawija, kusini mwa mkoa wa Kirkuk.

Kiongozi wa Daesh baada ya kukamatwa na wenzake

Katika hatua nyingine, Jabar al-Ma'amuri, mmoja wa viongozi wa harakati ya wananchi ya Hashdu sh-Sha'abi, amewapa hiari wanachama wa Daesh katika mji wa al-Hawija, ima wajisalimishe au waangamizwe. Mji wa al-Hawija ndio ngome ya mwisho ya kundi hilo la kigaidi la Daesh linalopata uungaji mkono kutoka Marekani, Saudia, Israel na baadhi ya nchi za eneo na za nje ya eneo.

Tags