-
Libya yaagiza kukamatwa maafisa 8 katika uchunguzi wa kuporomoka kwa bwawa
Sep 26, 2023 07:42Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Libya imesema, Mwendesha Mashtaka Mkuu huyo ameamuru kukamatwa maafisa wanane kama sehemu ya uchunguzi wake kuhusu maafa ya hivi majuzi ya mafuriko ambayo yalisababisha vifo vya maelfu ya watu.
-
UN: Wahajiri 400 wameaga dunia kwa mafuriko Libya
Sep 20, 2023 07:17Umoja wa Mataifa umesema mamia ya wahajiri ni miongoni mwa maelfu ya watu waliopoteza maisha kutokana na mafuriko makubwa yaliyosababishwa na kimbunga huko mashariki mwa Libya.
-
Hilali Nyekundu ya Iran yatuma misaada ya kibinadamu Libya
Sep 17, 2023 04:39Mkuu wa Shirika la Hlilali Nyekundu la Iran (IRCS) amesema jumuiya hiyo imetuma tani 40 za misaada ya dharura nchini Libya, kufuatia maafa makubwa ya roho na mali za watu yaliyosababishwa na mafuriko makubwa katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
-
UN: Baadhi ya watu nchini Libya wamepoteza wanafamilia 50 au zaidi
Sep 16, 2023 10:59Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA, Martin Griffiths amesema, umoja huo unaendelea kuhamasisha juhudi za utoaji misaada kwa nchi za Libya na Morocco kufuatia majanga mawili makubwa tofauti yaliyozikumba nchi hizo sambamba na machungu na maumivu makubwa yaliyozipata familia zilizofiwa na kupoteza wapendwa wao katika majanga hayo.
-
Meya wa Derna: Vifo vya mafuriko Libya yumkini vimepindukia 20,000
Sep 15, 2023 03:20Meya wa mji wa Derna, mashariki mwa Libya amesema huenda idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na athari za kimbunga kikali kilichoikumba nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika ikapindukia watu 20,000.
-
Spika wa Bunge la Iran aelezea masikitiko yake kwa serikali na watu wa Libya baada ya mafuriko
Sep 14, 2023 02:55Katika ujumbe wake kwa Spika mwezake wa Bunge la Libya, Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) ameelezea masikitiko yake kwa serikali na wananchi wa Libya kufuatia maafa makubwa ya roho na mali za watu yaliyosababishwa na mafuriko makubwa katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika
-
Rais wa Iran atuma salamu za rambirambi kwa taifa Libya kufuatia maafa ya mafuriko
Sep 12, 2023 14:14Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametuma salamu za rambirambi kwa Waziri Mkuu na wananchi wa Libya kutokana na vifo vya maelfu ya watu nchini huko vilivyosababishwa na Kimbunga Daniel kilichoikumba nchi hiyo na kuzusha mafuriko makubwa.
-
Kimbunga kikali cha Mediterrania, mafuriko yaua maelfu ya watu Libya
Sep 12, 2023 02:46Mamia ya watu wamepoteza maisha baada ya kimbunga kikali cha Mediterrania kupiga mashariki mwa Libya na kusababisha mvua kubwa na mafuriko.
-
Kupinga Waziri Mkuu wa Libya kuanzishwa uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel
Sep 02, 2023 10:45Baada ya maandamano makubwa ya wananchi wa Libya ya kulaaniwa kukutana na kufanya mazungumzo Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa nchi hiyo na mwenzake wa utawala wa Kizayuni, kwa mara nyingine tena Waziri Mkuu wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya, Abdel-Hamid al-Dbeibeh, alisisitiza siku ya Alkhamisi juu ya uungaji mkono wa nchi hiyo kwa kwa malengo matukufu ya Palestina na mapambano ya Palestina dhidi ya ya utawala haramu wa Israel.
-
Walibya: Serikali ya Dbeibah itimuliwe kwa kuvuka mistari myekundu
Aug 29, 2023 11:49Viongozi na wanasiasa mashuhuri wa Libya wametoa mwito wa kuondolewa mamlakani serikali nzima ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Abdul Hamid Dbeibah, baada ya kufichuka habari ya Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo kuonana kwa siri na waziri wa mambo ya nje wa utawala wa Kizayuni, Eli Cohen nchini Italia.