Libya yawafukuza mabalozi wa nchi kadhaa zinazounga mkono utawala wa Kizayuni
(last modified Thu, 26 Oct 2023 06:13:42 GMT )
Oct 26, 2023 06:13 UTC
  • Libya yawafukuza mabalozi wa nchi kadhaa zinazounga mkono utawala wa Kizayuni

Ikiwa ni katika hatua yake ya kupinga kuendelea jinai na mashambulizi ya kinyama ya utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wa Ukanda wa Ghaza, Libya imewatimua mabalozi wa nchi kadhaa zinazounga mkono utawala wa Kizayuni nchini humo.

Kwa mujibu wa ripoti ya IRNA siku ya Jumatano, Libya iliwatimua mabalozi wa Uingereza, Marekani, Ufaransa na Italia kutoka Tripoli, mji mkuu wa Libya kwa kuunga mkono jinai na mashambulizi ya utawala ghasibu wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza.

Uamuzi huo umechukuliwa baada ya Bunge la Libya kutangaza alasiri ya Jumatano kuondola haraka iwezekanavyo nchini humo mabalozi wa nchi zinazounga mkono jinai za utawala wa Kizayuni kufuatia kuendelea jinai na mashambulizi ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza na uungaji mkono wa nchi za Magharibi kwa jinai za utawala huo.

Katika uamuzi mwingine, Bunge la Libya limetaka kusitishwa mara moja uuzaji wa mafuta kwa nchi zinazounga mkono jinai za utawala wa Kizayuni.

Jinai za Wazayui Ghaza

Katika kukabiliana na jinai za Wazayuni, Jumamosi, Oktoba 7, 2023, vikosi vya muqawama wa Palestina vilianzisha operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa kutokea Ukanda wa Ghaza dhidi ya maeneo ya utawala wa Kizayuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.

Tangu kuanza kwa operesheni hiyo, jeshi la Kizayuni, ambalo halina uwezo wa kukabiliana moja kwa moja na wapiganaji wa muqawama, limekuwa likishambulia kwa mabomu maeneo ya makazi, hospitali, vituo vya kidini na shule huko Ghaza.

Kwa mujibu wa ripoti ya Wizara ya Afya ya Palestina, katika kipindi cha siku 19 za jinai za utawala wa Kizayuni katika ukanda huo, zaidi ya watu 6,000 wameuawa shahidi na takriban watu 20,000 wamejeruhiwa.