-
UN: Baadhi ya watu nchini Libya wamepoteza wanafamilia 50 au zaidi
Sep 16, 2023 10:59Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA, Martin Griffiths amesema, umoja huo unaendelea kuhamasisha juhudi za utoaji misaada kwa nchi za Libya na Morocco kufuatia majanga mawili makubwa tofauti yaliyozikumba nchi hizo sambamba na machungu na maumivu makubwa yaliyozipata familia zilizofiwa na kupoteza wapendwa wao katika majanga hayo.
-
Meya wa Derna: Vifo vya mafuriko Libya yumkini vimepindukia 20,000
Sep 15, 2023 03:20Meya wa mji wa Derna, mashariki mwa Libya amesema huenda idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na athari za kimbunga kikali kilichoikumba nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika ikapindukia watu 20,000.
-
Spika wa Bunge la Iran aelezea masikitiko yake kwa serikali na watu wa Libya baada ya mafuriko
Sep 14, 2023 02:55Katika ujumbe wake kwa Spika mwezake wa Bunge la Libya, Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) ameelezea masikitiko yake kwa serikali na wananchi wa Libya kufuatia maafa makubwa ya roho na mali za watu yaliyosababishwa na mafuriko makubwa katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika
-
Rais wa Iran atuma salamu za rambirambi kwa taifa Libya kufuatia maafa ya mafuriko
Sep 12, 2023 14:14Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametuma salamu za rambirambi kwa Waziri Mkuu na wananchi wa Libya kutokana na vifo vya maelfu ya watu nchini huko vilivyosababishwa na Kimbunga Daniel kilichoikumba nchi hiyo na kuzusha mafuriko makubwa.
-
Kimbunga kikali cha Mediterrania, mafuriko yaua maelfu ya watu Libya
Sep 12, 2023 02:46Mamia ya watu wamepoteza maisha baada ya kimbunga kikali cha Mediterrania kupiga mashariki mwa Libya na kusababisha mvua kubwa na mafuriko.
-
Kupinga Waziri Mkuu wa Libya kuanzishwa uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel
Sep 02, 2023 10:45Baada ya maandamano makubwa ya wananchi wa Libya ya kulaaniwa kukutana na kufanya mazungumzo Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa nchi hiyo na mwenzake wa utawala wa Kizayuni, kwa mara nyingine tena Waziri Mkuu wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya, Abdel-Hamid al-Dbeibeh, alisisitiza siku ya Alkhamisi juu ya uungaji mkono wa nchi hiyo kwa kwa malengo matukufu ya Palestina na mapambano ya Palestina dhidi ya ya utawala haramu wa Israel.
-
Walibya: Serikali ya Dbeibah itimuliwe kwa kuvuka mistari myekundu
Aug 29, 2023 11:49Viongozi na wanasiasa mashuhuri wa Libya wametoa mwito wa kuondolewa mamlakani serikali nzima ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Abdul Hamid Dbeibah, baada ya kufichuka habari ya Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo kuonana kwa siri na waziri wa mambo ya nje wa utawala wa Kizayuni, Eli Cohen nchini Italia.
-
Muqawama wa Palestina wawapongeza wananchi wa Libya
Aug 29, 2023 02:45Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imetoa shukrani rasmi kwa wananchi wa LIbya kwa hatua yao ya kuonesha msimamo imara wa kulaani hatua ya waziri wa mambo ya nje wa Libya ya kuonana na waziri wa mambo ya nje wa Israel.
-
Waziri wa Libya akimbia nchi baada ya kusimamishwa kazi, hasira zinaendelea
Aug 28, 2023 12:22Waziri wa Mambo ya Nje wa Libya, Najla al Mangoush amekimbilia Uturuki baada ya Mkuu wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya kumsimamisha kazi kwa kosa la kuonana na waziri wa mambo ya nje wa utawala wa Kizayuni nchini Italia.
-
Italia yazilaumu nchi za Magharibi kwa kuivamia kijeshi Libya wakati wa Gaddafi
Aug 18, 2023 04:36Waziri wa Mambo ya Nje ambaye pia ni Naibu Waziri Mkuu wa Italia amezilaumu nchi za Magharibi kwa kuivamia kijeshi Libya wakati wa harakati za wananchi za kuipindua serikali ya kiongozi wa muda mrefu Muammar Gaddafi lakini ameshindwa kulaumu uharibifu mkubwa uliofanywa na madola hayo ya Magharibi katika uvamizi wao huo.