-
Askari wa Ufaransa na Imarati wanaswa wakishirikiana na Haftar, Libya
Jun 28, 2019 03:13Askari wa Ufaransa na Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) wamekuwa wakishirikiana na wapiganaji wa kundi la Jenerali Khalifa Haftar linalopiganaji dhidi ya serikali inayotambuliwa rasmi kimataifa ya Libya.
-
Baada ya kupata pigo, hatimaye Jenerali Khalifa Haftar alazimika kukubali mazungumzo Libya
Jun 27, 2019 06:35Wapiganaji wanaojiita Jeshi la Taifa la Libya wamelazimika kukubali mazungumzo ya kuutafutia ufumbuzi mgogoro wa nchi hiyo ulioanzishwa na kundi hilo linaloungwa mkono na Saudi Arabia, Imarati, Misri na Ufaransa.
-
Jitihada za serikali ya Muafaka wa Kitaifa Libya za kukomesha mgogoro wa ndani
Jun 17, 2019 21:54Kutokana na kuendelea mgogoro na vita vya ndani nchini Libya na hali mbaya inayotawala nchini humo, kiongozi wa serikali ya Muafaka wa Kitaifa ametoa wito wa kuundwa Jukwaa la Libya kwa shabaha ya kutatua mgogoro wa nchi hiyo na kuunda baraza la mapatano ya kitaifa.
-
Fayez al-Sarraj ataka uchaguzi ufanyike Libya kabla ya kumalizika mwaka
Jun 17, 2019 03:19Waziri Mkuu wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya ametoa mwito wa kufanyika uchaguzi nchini humo kabla ya mwisho wa mwaka huu. Awali uchaguzi mkuu nchini humo ulikuwa umepangwa kufanyika Disemba 10 mwaka jana 2018 lakini zoezi hilo liliahirishwa kutokana mpasuko uliojitokeza baina ya viongozi wa mirengo hasimu ya kisiasa na wimbi la mapigano na machafuko yaliyozuka katika mji mkuu wa nchi hiyo, Tripoli.
-
Vikosi vya Jenerali muasi, Khalifa Haftar vyaua raia 9 Tripoli, Libya
Jun 16, 2019 03:20Kikosi cha Anga cha wapiganaji wa Jenerali Khalifa Haftar kimefanya shambulizi la anga lililolenga ghala la jeshi la Serikali ya Umoja wa Kitaifa inayoungwa mkono na jamii ya kimataifa katika mji mkuu Tripoli na kuua watu tisa.
-
UN: Raia 42 wameuawa katika mapigano nchini Libya
Jun 15, 2019 08:01Umoja wa Mataifa umesema mapigano baina ya vikosi vya kamanda muasi wa Libya, Jenerali Khalifa Haftar na Fayez al-Sarraj, Waziri Mkuu wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa inayoungwa mkono na jamii ya kimataifa katika mji mkuu Tripoli yamesababisha vifo vya raia 42, huku wengine zaidi ya 120 wakijeruhiwa.
-
Baraza la Usalama laongeza muda wa vikwazo kwa Libya kwa mwaka mmoja mwingine
Jun 10, 2019 22:49Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa mara nyingine tena limekipatia mamlaka kikosi cha Umoja wa Ulaya kuendesha mapambano dhidi ya silaha haramu kuelekea Libya na kutekeleza vikwazo vya silaha vilivyowekewa nchi hiyo iliyoathiriwa na machafuko ya kaskazini mwa Afrika.
-
UN: Hali ya wahajiri nchini Libya inatia wasiwasi sana + Video
Jun 09, 2019 22:04Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa hali ya wahajiri nchini Libya inatia wasiwasi mkubwa.
-
Wahajiri 2 waaga dunia, 25 watoweka katika ajali ya boti Libya
Jun 03, 2019 01:51Umoja wa Mataifa umesema kuwa wahajiri wawili wa Kiafrika wamekufa maji huku wengine 25 wakitoweka baada ya boti yao kuzama katika pwani ya Libya kwenye bahari ya Mediterrania, wakiwa katika safari hatarishi ya kuelekea Ulaya.
-
Droni ya Imarati yatunguliwa nchini Libya
Jun 02, 2019 23:48Jeshi la Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya limetangaza kuwa, limefanikiwa kutungua ndege moja isiyo na rubani (droni) ya serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) katika mji mkuu wa Libya, Tripoli.