-
Hatua za kiusalama zachukuliwa kukabiliana na genge la Daesh nchini Libya
May 19, 2018 09:25Viongozi wa serikali ya Libya wametangaza kuchukua hatua zaidi za kiusalama kwa ajili ya kukabiliana na kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) ndani ya nchi hiyo.
-
Trump: Huenda kiongozi wa Korea Kaskazini akapatwa na hatima kama ya Gaddafi
May 18, 2018 23:43Rais Donald Trump wa Marekani amemuonya kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un kuwa huenda akapatwa na hatima kama iliyomfika kiongozi wa zamani wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi, iwapo Pyongyang haitaachana na mradi wake wa silaha za nyuklia.
-
Watu 9 wauawa katika mapigano mapya mashariki mwa Libya
May 16, 2018 09:19Watu 9 wameuawa kwenye mapigano baina ya jeshi la Libya na magenge ya kigaidi katika mji wa Derna wa mashariki mwa nchi hiyo.
-
Mamia ya wahajiri haramu waokolewa katika pwani za magharibi mwa Libya
May 13, 2018 11:16Wahajiri haramu wapatao 340 raia wa nchi tofauti za Afrika wameokolewa katika pwani za magharibi mwa Libya.
-
Watu kadhaa wauawa na kujeruhiwa katika mapigano mapya kusini mwa Libya
May 12, 2018 09:39Watu kadhaa wameuawa na kujeruhiwa katika mapigano mapya yaliyotokea katika mji wa Sabha, kusini magharibi mwa Libya.
-
ICC yataka msaada wa Baraza la Usalama kumkamata Seiful Islam Gaddafi
May 10, 2018 09:57Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC imeliomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuisaidia katika kuwakamata watu watatu wanaosakwa nchini Libya akiwemo Seiful Islam, mwana wa kiume wa aliyekuwa kiongozi wa wa nchi hiyo, Kanali Muammar Gaddafi.
-
Watu wawili wauawa katika shambulizi ya kujiripua mashariki mwa Libya
May 09, 2018 03:22Afisa mmoja wa ngazi za juu wa usalama wa Libya amesema kuwa, watu wawili wameuawa mashariki mwa nchi hiyo baada ya gaidi mmoja kujiripua katika kituo cha upekuzi cha "Jeshi la Taifa la Libya" linaloongozwa na Jenerali Khalifa Haftar.
-
Operesheni ya kuukomboa mji wa Derna yaanza nchini Libya
May 07, 2018 20:56Kamanda wa timu ya operesheni ya jeshi la Libya katika mji wa Derna wa kaskazini mashariki mwa nchi hiyo amesema kuwa, operesheni ya kuukomboa mji huo kutoka mikononi mwa genge moja la kigaidi ilianza rasmi jana (Jumatatu).
-
Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya yatoa wito wa kuondolewa vikwazo vya silaha
May 05, 2018 10:22Waziri wa Mambo ya Nje wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya ameiomba jamii ya kimataifa iunge mkono takwa la serikali hiyo la kuondolewa vikwazo vya silaha na zana za kijeshi inazozihitaji.
-
Uungaji mkono wa Serikali ya Maafikiano ya Kitaifa ya Libya kwa takwa la kamati ya pande nne
May 03, 2018 02:30Serikali ya Maafikiano ya Kitaifa ya Libya imetangaza uungaji mkono wake kwa takwa la kamati ya pande nne la kuyakubali matokeo ya uchaguzi ujao katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.