-
Maandamano yashtadi US baada ya raia mwingine kuuawa Minneapolis
Jan 25, 2026 03:29Maajenti wa serikali kuu ya Marekani wamemuua kwa kumpiga risasi mtu mwingine mjini Minneapolis huku kukiwa na msako mkali dhidi ya wahamiaji, na kushadidisha maandamano na wito mpya kwa Rais Donald Trump kuwaondoa mara moja maafisa hao waliojizatiti kwa silaha katika jiji hilo lililoko katika jimbo la Minnesota.
-
Trump aitishia Canada kwa ushuru wa 100%, kisa biashara na China
Jan 25, 2026 03:27Rais wa Marekani, Donald Trump ametishia kuitoza Canada ushuru wa asilimia 100 iwapo Waziri Mkuu wa Canada, Mark Carney atatekeleza makubaliano ya kibiashara na China.
-
DA yakanusha madai ya Trump ya kuwepo mauaji ya Wazungu A/Kusini
Jan 23, 2026 23:18Kiongozi wa chama cha Democratic Alliance cha Afrika Kusini (DA), John Steenhuisen amekadhibisha madai ya kuwepo "mauaji ya kimbari ya Wazungu" nchini Afrika Kusini.
-
Kwa nini rais wa Brazil amemkejeli Trump?
Jan 23, 2026 23:17Rais Lula da Silva wa Brazil amemkejeli Rais Donald Trump wa Marekani kutokana na tweet nyingi za kutatanisha anazoandika katika mitandao ya kijamii.
-
Kamanda mwandamizi wa Jeshi la Iran amuonya vikali Trump
Jan 22, 2026 03:26Kamanda wa ngazi ya juu wa jeshi la Iran amemuonya vikali Rais Donald Trump wa Marekani kufuatia matamshi yake ya hivi karibuni ya vitisho dhidi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei.
-
Putin: Denmark imekuwa ikiitazama Greenland kama koloni lake
Jan 22, 2026 02:31Rais wa Russia, Vladimir Putin amesema, Denmark imekuwa ikiichukulia Greenland kama koloni lake. Amesema hayo akitoa mtazamo wake kuhusu mpango wa Rais wa Marekani, Donald Trump wa 'kukinunua' kisiwa hicho cha Aktiki kinachojitawala.
-
Bunge la EU lasimamisha makubaliano ya biashara na US; kisa vitisho vya Trump
Jan 22, 2026 02:21Bunge la Ulaya limesimamisha rasmi mchakato wa kuidhinisha makubaliano yake ya kibiashara na Marekani, kutokana na vitisho vya Rais Donald Trump vya kutoza ushuru wa asilimia 10 kwa bidhaa za EU zinazoenda Marekani, iwapo umoja huo hautaafiki azma ya Washington ya kuitwaa Greenland.
-
Mahakama ya Kimataifa ya Jinai chini ya kivuli cha undumakuwili wa Marekani
Jan 22, 2026 00:56Naibu mwakilishi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa ametishia kuichukulia hatua zaidi Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC iwapo itaendeleza uchunguzi wake kuhusu uhalifu na jinai za nchi hiyo.
-
Pentagon kutuma wanajeshi 1,500 kukabiliana na waandamanaji Minnesota
Jan 18, 2026 23:10Wizara ya Vita ya Marekani (Pentagon) imewaamuru wanajeshi wapatao 1,500 walio kazini wawe tayari kutumwa kwenda kukandamiza maandamano huko Minnesota.
-
Wakazi wa Greenland waandamana kupinga vitisho vya Trump
Jan 18, 2026 06:54Wakazi wa Greenland walifanya maandamano jana Jumamosi kupinga azma ya Rais wa Marekani Donald Trump ya kutaka kisiwa hicho cha Aktiki kikabidhiwe Washington, wakisisitiza kuwa wakazi wa eneo hilo wanapasa kuachwa waamue mustakabali wa kisiwa hicho.