-
Mamlaka za Ghaza zairejeshea Israel miili 88 ya Wapalestina isiyo na 'utambulisho' wowote
Sep 26, 2024 01:42Mamlaka za Palestina katika Ukanda wa Ghaza zimeurejeshea utawala wa Kizayuni wa Israel kontena lililobeba miili ya Wapalestina 88 ambayo haitambuliki kutokana na kutoambatanishwa na taarifa zozote kuhusu utambulisho wao.
-
Marekani kuiuzia Misri makombora ya dola milioni 740
Sep 26, 2024 00:29Serikali ya Marekani imeidhinisha mauzo ya makombora yenye thamani ya mamilioni ya dola kwa Misri licha ya serikali ya nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika kuendelea kuandamwa na shutuma za ukiukaji wa haki za binadamu.
-
Iran: Marekani inataka kushadidisha taharuki katika eneo
Sep 26, 2024 00:29Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, Marekani pamoja na Israel zinafuatilia kuyumbisha uthabiti na usalama wa eneo la Magharibi mwa Asia, na kupanua mvutano na mgogoro katika eneo hili.
-
Tuhuma na misimamo ya kurudiwarudiwa ya Marekani kwa ulimi wa Joe Biden katika Umoja wa Mataifa
Sep 26, 2024 00:28Jumanne ya wiki hii, rais wa Marekani, Joe Biden, alitoa hotuba yake ya mwisho katika kikao cha 79 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York na kukariri madai ya uongo ya siku zote dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na dhidi ya kambi ya Muqawama. Rais wa Marekani alidai kuwa eti serikali yake inapigania kuleta amani na utulivu katika ukanda wa Asia Magharibi.
-
Rais wa Iran: Amani inapasa kuchukua nafasi ya vita duniani
Sep 23, 2024 23:58Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, amani na usalama vinapaswa kuchukua nafasi ya vita na umwagaji damu duniani. Rais Masoud Pezeshkian amesema hayo alipoona na wakurugenzi waandamizi wa vyombo vya habari vya Marekani mjini New York na kubainisha kwamba, Iran sio kama vyombo vya habari vya dunia vinavyoinyesha na tuko tayari kuishi kwa amani na usalama na dunia nzima.
-
Akthari ya wananchi wa Marekani wanataka nchi yao irejee katika mapatano ya JCPOA
Sep 23, 2024 22:49Watu wengi nchini Marekani wanataka Washington irudi katika Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA). Hii ni kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni uliofanyika huko Marekani.
-
Kila saa moja linaripotiwa tukio la ubakaji katika mji mkuu wa Uingereza, London
Sep 23, 2024 03:38Takwimu zilizotolewa na Polisi ya Uingereza zinaonyesha kuwa tukio moja la ubakaji huwa linaripotiwa kila saa katika mji mkuu wa nchi hiyo London.
-
Kan'ani: Marekani ndiyo inayopaswa kubeba dhima ya jinai za Israel huko Palestina, Lebanon na Syria
Sep 21, 2024 23:29Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya ya Iran amesema kuwa, Marekani ndiyo inayopaswa kubeba dhima na kujibu malalamiko makubwa ya kimataifa kwa kushiriki kwake katika jinai za utawala wa Kizayuni huko Palestina, Lebanon na Syria.
-
Msaada wa EU kwa Ukraine tangu vilipoanza vita na Russia 2022 umefikia dola bilioni 131
Sep 18, 2024 02:32Misaada iliyotolewa na Umoja wa Ulaya (EU) na nchi wanachama wa umoja huo kwa Ukraine tangu vilipoanza kati ya nchi hiyo na Russia mnamo Februari 2022 imefikia yuro bilioni 118 (dola bilioni 131). Hayo yameelezwa na Makamu wa Rais wa Tume ya EU Valdis Dombrovskis.
-
Kuendelea visa vya watu kujichoma moto huko Marekani; nembo ya kupinga vita vya Ukanda wa Gaza
Sep 16, 2024 07:47Raia mmoja wa Marekani aliyejulikana kwa jina na Matt Nelson amejichoma moto katika mji wa Boston akipinga na kulalamikia vita vya Israel dhidi ya watu wa Gaza.