-
Iran: Baka la aibu la Mapinduzi ya kijeshi ya 1953 litabakia milele kwenye mapaji ya nyuso za US na UK
Aug 18, 2024 08:45Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema, baka la aibu la kuiondoa madarakani Serikali halali ya Iran iliyochaguliwa na wananchi, kupitia mapinduzi ya kijeshi ya tarehe 28 Mordad 1332 (Agosti 19, 1953) na la kuuhami Udikteta kisiasa, kiusalama na kijeshi litaendelea kubakia milele kwenye mapaji ya nyuso za tawala za Marekani na Uingereza.
-
China: Marekani ndio tishio kubwa zaidi la nyuklia duniani
Aug 17, 2024 06:57Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya China amesema, Marekani ndiyo hatari kubwa zaidi kwa dunia endapo yatatokea mapigano ya nyuklia.
-
Wanachuo wanaoitetea Palestina 'wakaribisha' kujiuzulu Rais wa Chuo Kikuu cha Columbia
Aug 15, 2024 04:25Rais wa Chuo Kikuu cha Columbia Minouche Shafik alitangaza kujiuzulu jana Jumatano, takriban miezi minne baada ya chuo hicho kushuhudia maandamano ya wananchuo waliokuwa wakilalamikia vita vya mauaji ya kimbari vya utawala wa Israel huko Gaza.
-
Kikao cha Baraza la Usalama kuhusu vita vya Ghaza; makabiliano ya Marekani na Jamii ya Kimataifa
Aug 14, 2024 07:45Kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa cha kujadili shambulio la utawala wa Kizayuni dhidi ya Skuli ya Al-Tabeen katika Ukanda wa Ghaza kilifanyika siku ya Jumanne ambapo akthari ya wanachama wa Baraza hilo walilaani jinai ya utawala huo na kusisitiza juu ya ulazima wa kusitishwa vita mara moja huko Ghaza.
-
Iran: Marekani ndiye muungaji mkono na muenezaji mkuu wa ugaidi katika eneo na dunia
Aug 13, 2024 02:11Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesema, Marekani ndiyo muungaji mkono na muenezaji mkuu wa ugaidi katika eneo na dunia.
-
CAIR yamtaka Biden 'alaani' ugaidi wa kiserikali wa Israel
Aug 11, 2024 04:04Baraza la Mahusiano ya Kiislamu Marekani (CAIR) limemtaka Rais Joe Biden wa nchi hiyo ajibu na kulaani vitendo vya ugaidi wa kiserikali vinavyofanywa na utawala haramu wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.
-
Muqawama: US ni mshiriki wa mauaji mapya ya halaiki Gaza
Aug 10, 2024 07:43Makundi ya mrengo wa Muqawama katika eneo la Asia Magharibi yamelaani vikali jinai mpya ya kuogofya ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza, ambapo zaidi ya Wapalestina 100 wameuawa shahidi na makumi ya wengine kujeruhiwa.
-
Iran yakadhibisha madai ya kutaka kuingilia uchaguzi wa Marekani
Aug 10, 2024 07:42Ofisi ya uwakilishi wa kudumu ya Iran katika Umoja wa Mataifa imepuuzilia mbali madai kuwa Jamhuri ya Kiislamu inakula njama ya kuathiri matokeo ya uchaguzi wa rais wa Marekani utakaofanyika baadaye mwaka huu.
-
Sanders: Wamarekani hawaungi mkono vita vya kikatili vya Netanyahu
Aug 09, 2024 04:13Seneta moja mashuhuri nchini Marekani kwa mara nyingine ametoa mwito wa kusitishwa vita mara moja katika Ukanda wa Gaza akisisitiza kuwa, wananchi wa Marekani hawaungi mkono jinai na vita vya Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israel dhidi ya wakazi wa eneo hilo la Palestina lililozingirwa na linalokaliwa kwa mabavu.
-
WHO yachukua hatua dhidi ya kirusi cha Mpox huku kesi za maambukizi zikiongezeka Afrika
Aug 08, 2024 04:22Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus, ameitisha mkutano wa dharura wa wataalamu wa kimataifa huku kesi za maambukizi ya spishi hatari zaidi ya kirusi cha Mpox zikiongezeka katika nchi za Afrika.