Aug 13, 2024 05:41 UTC
  • Iran: Marekani ndiye muungaji mkono na muenezaji mkuu wa ugaidi katika eneo na dunia

Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesema, Marekani ndiyo muungaji mkono na muenezaji mkuu wa ugaidi katika eneo na dunia.

Amir Saeed Irvani, ameyasema hayo katika barua aliyomwadikia Rais wa Baraza la Usalama na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akijibu tuhuma za Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwamba inaunga mkono ugaidi katika eneo na kubainisha kuwa, inachekesha na inaaibisha kwa Marekani kutoa tuhuma hizo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wakati huohuo ikiwa inaunga mkono na kusaidia mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala wa Israel, huku ikiwa mtetezi mkuu wa utawala huo.
 
Irvani amekanusha tuhuma hizo zisizo na msingi na kulaani mienendo ya kutowajibika ya mwakilishi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa na kueleza kwamba, misaada ya silaha ya Marekani kwa Wazayuni ni kwa ajili ya kuendeleza mauaji ya Wapalestina wasio na hatia wakiwemo watoto na wanawake.
Amir Saeed Irvani

Ameongeza kuwa, jinai ya karibuni zaidi ya utawala wa Israel dhidi ya raia wasio na makazi katika Skuli ya Al-Tabeen katikati ya mji wa Ghaza mnamo Jumamosi, Agosti 10, 2024, ambayo ilipelekea kuuawa shahidi Wapalestina wasio na hatia wasiopungua 100, wakiwemo watoto na wanawake, ni matokeo ya uungaji mkono huohuo wa Marekani usio na udadisi wowote.

 
Mwakilishi wa Iran katika Umoja wa Mataifa pia amesema, uungaji mkono wa Marekani kwa makundi ya kigaidi yaliyoorodheshwa na Umoja wa Mataifa kama vile Jabhat al-Nusra katika maeneo yaliyovamiwa na kukaliwa kwa mabavu na Marekani yenyewe ndani ya Jamhuri ya Kiarabu ya Syria ni ukiukaji wa wazi wa Hati ya Umoja wa Mataifa, sheria za kimataifa na maazimio ya Baraza la Usalama.../

 

Tags