-
Kufukuzwa Manowari ya Marekani kutoka kwenye maji ya China
Nov 26, 2023 23:14Ingawa muda mrefu haujapita tangu kufanyika kikao kati ya marais wa Marekani na China mjini San Francisco, kikao ambacho Rais Joe Biden wa Marekani alikitaja kuwa chanya, Tian Junli, Msemaji wa Kamandi ya Pamoja ya Vikosi vitatu vya Jeshi la Nchi Kavu, Anga na Baharini vya Jeshi la China ametangaza kufukuzwa manowari ya Marekani kutoka kwenye eneo la maji ya nchi hiyo.
-
Harakati ya Fat'h ya Iraq: Vita dhidi ya Wazayuni ndio kwanza vimeanza
Nov 26, 2023 08:33Mjumbe wa Muungano wa al Fat'h wa Iraq ameashiria jinsi makundi ya muqawama ya nchi hiyo yanavyoyaunga mkono makundi ya muqawama ya Palestina katika vita vya Ghaza na kusema kuwa, makundi hayo yataendelea kushambulia vituo vya wanajeshi vamizi wa Marekani nchini Iraq.
-
Al-Khazali: Marekani haitaki kuondoka Iraq, inatumia kisingizio cha kupambana na Daesh
Nov 25, 2023 09:33Kiongozi wa harakati ya muqawama ya Iraq amesema kuwa, vikosi vya majeshi ya Marekani havina nia ya kuondoka katika nchi hiyo ya Kiarabu na vinahalalisha uwepo wao kinyume cha sheria kwa kutumia kisingizio cha kupambana na kundi la kigaidi la Daesh ambalo limekwishakufa na kutoweka.
-
Amir-Abdollahian: Uungaji mkono wa Marekani kwa Israel ulisababisha kuendelea kwa vita Gaza
Nov 24, 2023 08:32Waziri wa Mashauriano ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kama si msaada na himaya ya Marekani kwa utawala ghasibu wa Israel, utawala huo bandia haungeweza kuendeleza vita na Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (HAMAS).
-
70% ya vijana Marekani wanapinga Biden kuikingia kifua Israel
Nov 23, 2023 04:03Uchunguzi mpya wa maoni uliofanywa nchini Marekani unaonyesha kuwa, aghalabu ya vijana nchini humo hawaungi mkono msimamo wa Rais Joe Biden kwa mashambulizi ya mabomu, jinai za kivita na uporoaji wa ardhi unaofanywa na utawala haramu wa Israel dhidi ya Palestina.
-
Maelfu ya Wamarekani waandamana kupinga siasa za Biden
Nov 18, 2023 03:53Maelfu ya Wamarekani wamekusanyika mbele ya Ikulu ya White House na New York kupinga siasa za Biden za kuunga mkono jinai za utawala wa kibaguzi wa Israel.
-
Iran: US ndiyo sababu ya kushtadi mgogoro Ukanda wa Gaza
Nov 18, 2023 00:19Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu haitaki vita vya Gaza vipanuke, lakini yumkini vitasambaa zaidi katika maeneo mengine kwa kuwa Marekani inachochea mgogoro huo kwa kuuunga mkono utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
WSJ: Rais Biden anakabiliwa na uasi ndani ya serikali kwa sababu ya himaya yake kwa Israel
Nov 16, 2023 10:01Jarida la Wall Street Journal limeripoti kuwa Rais wa Marekani, Joe Biden, anakabiliwa na uasi kutoka kwa baadhi ya taasisi za serikali yake zinazopinga uungaji mkono wake kwa Israel katika vita vyake dhidi ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas).
-
Biden, Blinken, na Austin washtakiwa mahakamani kwa kushindwa kuzuia mauaji ya kimbari huko Gaza
Nov 14, 2023 11:08Kituo cha Haki za Kikatiba nchini Marekani kimewasilisha kesi mahakamani dhidi ya Rais Joe Biden, Waziri wa Mambo ya Nje, Anthony Blinken na Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin kwa tuhuma za kutoa uungaji mkono usio na masharti kwa mauaji ya halaiki yaliyofanywa na Israel dhidi ya watu wa Palestina katika Ukanda wa Gaza.
-
Mabilionea wa Marekani kuendesha kampeni ya vyombo vya habari ili kuisafisha Israel na kuichafua HAMAS
Nov 13, 2023 22:55Bilionea mmoja mfanyabiashara nchini Marekani ameanzisha kampeni ya kuchangisha mamilioni ya dola ili kuvitumia vyombo vya habari visafishe sura chafu ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel sambamba na kuchafua haiba ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS, wakati maandamano ya kuunga mkono Palestina dhidi ya Israel yaknazidi kupamba moto ulimwenguni kote.