CNN: Marekani inatazamia kutuma Ukraine msaada mkubwa zaidi kabla ya 2025
https://parstoday.ir/sw/news/world-i107444-cnn_marekani_inatazamia_kutuma_ukraine_msaada_mkubwa_zaidi_kabla_ya_2025
Televisheni ya CNN yenye makao yake nchini Marekani imeripoti kuwa Washington inatazamia kutuma msaada mubwa zaidi huko Ukraine kabla ya Januari mwaka 2025 na kukfanyika uchaguzi wa rais nchini humo.
(last modified 2024-01-20T23:09:05+00:00 )
Jan 20, 2024 23:09 UTC
  • CNN: Marekani inatazamia kutuma Ukraine msaada mkubwa zaidi kabla ya 2025

Televisheni ya CNN yenye makao yake nchini Marekani imeripoti kuwa Washington inatazamia kutuma msaada mubwa zaidi huko Ukraine kabla ya Januari mwaka 2025 na kukfanyika uchaguzi wa rais nchini humo.

CNN imeripoti kuwa, Rais Joe Biden wa Marekani na Kongresi ya nchi hiyo walianza kujadili suala hilo tangu mwaka jana wa 2023. Rais wa Marekani ameomba kuendelezwa misaada ya kijeshi kwa ajili ya Ukraine yenye thamani ya dola bilioni 61 hata hivyo wabunge wa chama cha Republican katika Bunge la Wawakilishi la nchi hiyo mkabala wake wametaka kushadidishwa wazi wazi sera ya Biden kuhusu uhamiaji.  

Hii ni katika hali ambayo washauri wa Joe Biden pia wamewaonya wabunge kwamba Russia inaweza kushinda vita vya Ukraine ndani ya wiki au miezi kadhaa tu iwapo Kongresi  ya Marekani haitakubali kutenga fedha mpya kwa ajili ya Kyiv.  

Pamoja na juhudi hivi tajwa za Marekani za kuiunga mkono Ukraine, Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa Sébastien LeCorneau alikiri Ijumaa kwamba baadhi ya raia wa Ufaransa tayari wamejiandikisha kwa ajili ya kujiunga na jeshi la Ukraine dhidi ya Russia; matamshi ambayo yanaonekana kupingana  madai ya awali ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa kwamba Paris haina mamluki Kyiv au popote pengine. 

Hii ni katika hali ambayo White House, Muungano wao KIjeshi wa Nchi za Magharibi (NATO) na serikali ya Kyiv  zinajua vyema kwamba ikiwa Donald Trump atashinda uchaguzi wa mwezi Novemba, kuna uwezekano mkubwa akasimamisha msaada kwa Ukraine.