-
Msumbiji yatuma timu ya madaktari kutambua wahanga wa shambulio la kigaidi huko Palma
Apr 09, 2021 15:52Msemaji wa jeshi la Msumbiji amesema kuwa nchi hiyo inatuma timu ya madaktari ili kutambua miili ya watu 12 waliouawa katika shambulio la magaidi wenye uhusiano na kundi la Daesh katika machimbo ya gesi asilia kwenye mji wa Palma kaskazini mwa Msumbiji.
-
Viongozi wa SADC wanakutana kujadili vita dhidi ya ugaidi Msumbiji
Apr 08, 2021 02:34Viongozi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Kusini mwa Afrika, SADC, wanakutana leo katika mazungumzo ya dharura kuhusu mzozo unaoendelea nchini Msumbiji.
-
Raia 50 wa Afrika Kusini watoweka kufuatia shambulio la kigaidi Msumbiji
Apr 04, 2021 10:58Afrika Kusini imesema raia wake zaidi ya 50 hawajulikani walipo mpaka sasa baada ya magaidi kuvamia na kuudhibiti mji wa Pwani wa Palma nchini Msumbiji, huku taarifa zikisema kuwa makumi ya watu wameuawa katika shambulio hilo.
-
AU: Hatua za dharura zichukuliwe kuinusuru Msumbiji
Apr 01, 2021 10:40Umoja wa Afrika (AU) umetoa mwito wa kuchukuliwa hatua za dharura katika ngazi za kieneo na kimataifa kufuatia kushtadi harakati na mashambulio ya magenge ya kigaidi kaskazini mwa Msumbiji.
-
Msumbiji yaanzisha oparesheni kubwa ya kukomboa mji wa Palma
Mar 29, 2021 11:37Wizara ya Ulinzi ya Msumbiji imetangaza kuwa, jeshi la nchi hiyo limeanzisha oparesheni kubwa ya kukomboa mji wa pwani wa Palma unaodhibitiwa na kundi linalojiita al Shabab.
-
Save the Children: Magaidi wanaua watoto kwa kuwachinja Msumbiji
Mar 17, 2021 04:33Shirika la misaada ya kibinadamu la Save the Children limesema wanachama wa magenge ya kigaidi katika mkoa wa Cabo Delgado kaskazini mwa Msumbiji wanaua watoto wadogo kikatili kwa kuwakata vichwa.
-
Wanamgambo wenye silaha wakishambulia kituo cha gesi kaskazini mwa Msumbiji
Dec 30, 2020 07:27Kundi la watu wenye silaha wamekishambulia kijiji kimoja karibu na mradi mkubwa wa gesi wa Ufaransa kaskazini mwa Msumbiji.
-
UNICEF: Watoto 250,000 wamekimbia makazi Cabo Delgado , Msumbiji
Dec 23, 2020 00:53Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema takribani watoto 250,000 wamekimbia makazi yao kutokana na hujuma za kigaidi zinazoendelea kwenye jimbo la Cabo Delgado kaskazini mwa Msumbiji na sasa wako hatarini kupata magonjwa ya kuambukiza kwa kuwa msimu wa mvua unaanza.
-
UN yatiwa wasiwasi na mapigano Msumbiji; laki 4 wahama makazi yao
Dec 14, 2020 12:22Umoja wa Mataifa umetahadharisha kuwa, mgogoro mkubwa wa kibinadamu unanukia kaskazini mwa Msumbiji, ambapo watu zaidi ya laki nne wamelazimika kuyahama makazi yao wakihofia usalama wao.
-
Zaidi ya 50 wauawa kwa kukatwa vichwa na magaidi huko Msumbiji
Nov 10, 2020 07:21Makumi ya watu wakiwemo vijana mabarobaro wameuawa kwa kukatwa vichwa na genge la wanamgambo wenye mfungamano na kundi la kigaidi la Daesh (ISIS), kaskazini mashariki mwa Msumbiji.