Dec 30, 2020 07:27 UTC
  • Wanamgambo wenye silaha wakishambulia kituo cha gesi kaskazini mwa  Msumbiji

Kundi la watu wenye silaha wamekishambulia kijiji kimoja karibu na mradi mkubwa wa gesi wa Ufaransa kaskazini mwa Msumbiji.

Maafisa wa serikali ya Msumbiji wametangaza kuwa; jana Jumanne kundi la kigaidi la Daesh lilikishambulia kijiji kimoja karibu na mradi mkubwa wa gesi huko Monjane katika mkoa wa Cabo Delgado kaskazini mwa Msumbiji; mradi ambao Shirika la Gesi la Total la Ufaransa pia lina ubia.  

Mkoa wa Cabo Delgado ulioathiriwa na mashambulizi 

Maafisa husika wa Msumbiji wamelitaja kundi la kigaidi la Daesh kuwa ndilo lililohusika na shambulio hilo. 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kabla ya shambulio la jana, miaka miwili iliyopita pia mnamo mwezi Mei mwaka 2018 kijiji cha Monjane kilikumbwa na mashambulizi ya kadhaa ya makundi ya kigaidi. Miili ya watu kumi wakiwemo watoto wadogo ilipatikana katika eneo palipojiri mashambulizi hayo. 

Tangu mwezi Oktoba 2017, makundi ya kigaidi ambayo katika eneo hilo yanajulikana kwa jina la Al Shabab yalianzisha mashambulizi makubwa katika mkoa huo ambao akthari ya wakazi wake ni Waislamu. 

Viongozi wa serikali ya Msumbiji wameeleza kuwa, jumla ya watu 570,000 wamelazimika kuyahama makazi yao kufuatia mashambulizi ya makundi hayo ya kigaidi; na Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa (Unicef) pia umetangaza kuwa watoto 250,000 ni miongoni mwa wakimbizi hao tajwa. 

Tags