-
Watoto Karibu Laki Nne Msumbiji wanahitaji msaada, mvua kuendelea
Apr 28, 2019 14:32Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF limeonya kwamba watoto na familia zao nchini Msumbiji wanaweza kukabiliwa na hatari ya kifo kutokana na mafuriko makubwa na maporomoko.
-
Kimbunga cha Kenneth kufika kusini mwa Tanzania usiku wa leo, tahadhari zachukuliwa + Sauti
Apr 25, 2019 16:42Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Tanzania (TMA) imetangaza kuwa, kimbunga Kenneth kimeongezeka kasi na kinatarajiwa kufika pwani ya kusini ya Tanzania na kaskazini mwa Msumbiji kuanzia usiku wa leo. Hadi sasa wameshapokelewa watu takribani mia sita katika eneo la hifadhi. AMARI DACHI na taarifa zaidi akiripoti kutoka Dar es Salaam
-
UNICEF: Watoto milioni 1.5 wanahitaji msaada kusini mwa Afrika kufuatia Kimbunga Idai
Apr 15, 2019 07:48Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, limetoa ombi la dola milioni 1.6 kusaidia watoto takribani milioni 1.5 ambao wameathiriwa vibaya na Kimbunga Idai katika nchi za kusini mwa Afrika ambazo ni Msumbiji, Malawi na Zimbabwe.
-
Zaidi ya watu 1000 wamekumbwa na ugonjwa wa kipindupindu nchini Msumbiji
Apr 02, 2019 13:50Viongozi wa idara ya Msumbiji wametangaza kwamba zaidi ya watu 1000 wameambukizwa maradhi ya kipindupindu nchini humo.
-
Waliofariki dunia katika Kimbunga Idai wafika 746, maelfu wapoteza makazi
Mar 30, 2019 16:00Mamia ya maelfu ya watu wanahitaji misaada ya dharura ya chakula, maji na makazi baada ya Kimbunga Idai kusababisha uharibifu mkubwa Msumbiji, Zimbabwe na Malawi.
-
Baada ya mafuriko Msumbiji, WMO yatahadharisha kuhusu mabadiliko ya tabianchi
Mar 28, 2019 07:58Shirika la Umoja wa Mataifa la Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani (WMO) limesema dalili za wazi na athari za kiuchumi na kijamii zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi zinazongezeka kote duniani kukishuhudiwa kiwango kikubwa cha hewa chafuzi ya viwandani inayosababisha ongezeko la joto na kufikia viwango vya hatari.
-
Misaada ya UNCHR yaanza kuwasili Msumbiji baada ya mafuriko
Mar 28, 2019 07:57Ndege ya Shirika la kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR yenye msaada kwa watu walioathiriwa na kimbunga cha Idai imewasili Maputo, Msumbuji.
-
WHO yatahadharisha kuhusu kuibuka maradhi ya kipindupindu nchini Msumbiji
Mar 27, 2019 07:42Shirika la Afya Duniani (WHO) limetahadharisha kuhusiana na kuibuka wimbi la pili la maradhi ya kipindupindu na maradhi mengine katika nchi ya Msumbiji iliyopigwa na kimbunga cha Idai hivi karibuni.
-
Msaada wa dola milioni 20 kufuatia maafa ya mafuriko kusini mwa Afrika
Mar 21, 2019 07:40Watu zaidi ya 500 wamthibitishwa kupoteza maisha Zimbabwe, Malawi na Msumbiji kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na kimbuga Idai na kuwaacha maelfu bila makazi na hivyo wanahitaji msaada wa dharura wa kibinadamu. Kufuatia hali hiyo, mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa umetangaza kutoa msaada wa dola milioni 20 kusaidia waathirika.
-
Kimbunga cha Idai chaua zaidi ya watu 100 Zimbabwe na Msumbiji
Mar 18, 2019 07:56Watu zaidi ya 100 wameaga dunia na wengine wengi hawajulikani waliko katika nchi za Msumbiji na Zimbabwe baada ya kimbunga cha tropiki cha Idai kuzikumba nchi hizo za kusini mwa Afrika na kusababisha mafuriko ya gharika na pepo kali.