-
Magenge yenye silaha yauwa watu 30 katika muda wa siku 3 huko Benue, Nigeria
Nov 26, 2024 02:54Watu wasiopungua 30 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mashambulizi ya magenge yenye silaha yaliyojiri kwa muda wa siku tatu dhidi ya wakulima jamii mbalimbali katika jimbo la Benue kaskazini kati nchini Nigeria.
-
Wanajeshi wasiopungua 12 wa Nigeria wauawa katika hujuma ya Boko Haram
Nov 20, 2024 12:07Wanajeshi zaidi ya 12 wa Nigeria waliuliwa jana Jumanne katika mashambulizi kadhaa ya kundi la kigaidi la Boko Haram dhidi ya kambi ya jeshi katika jimbo la Borno kaskazini mwa nchi hiyo.
-
Jeshi la Nigeria laua 'magaidi' 187 ndani ya wiki moja
Nov 03, 2024 06:16Zaidi ya watu 187 wanaoshukiwa kuwa magaidi wameuawa huku wengine 262 wakikamatwa katika operesheni mbalimbali za kupambana na ugaidi za jeshi la Nigeria nchini kote katika muda wa wiki moja iliyopita.
-
Wabeba silaha waua wanakijiji 15 katika jimbo la Benue, Nigeria
Nov 01, 2024 09:39Kwa akali watu 15 wameuawa katika shambulizi la 'majambazi' waliojizatiti kwa silaha katika jimbo la Benue katikati mwa Nigeria.
-
Wahanga wa mlipuko wa lori la mafuta Nigeria wazikwa kwa umati
Oct 17, 2024 07:58Maafisa wa serikali za mitaa kaskazini mwa Nigeria jana waliungana na mamia ya waombolezaji katika mazishi ya maziko ya umati ya zaidi ya wahanga 140 waliopoteza maisha katika mlipuko mkubwa wa lori la mafuta usiku wa kuamkia jana.
-
Watu 21 wafariki dunia baada ya boti kugongana nchini Nigeria
Oct 09, 2024 07:03Polisi ya Nigeria jana ilithibitisha kupoteza maisha takriban watu 21 baada ya boti mbili za abiria ambazo hazikuwa zimesajiliwa kupinduka. Boti hizo zilipinduka baada ya kugongana katika jimbo la Lagos nchini Nigeria.
-
Mwanaharakati Nigeria: Kimbunga cha al-Aqsa kilianika udhaifu wa Israel
Oct 07, 2024 06:17Mwanaharakati mashuhuri wa haki za binadamu nchini Nigeria amesema Operesheni ya Kimbunga cha al-Aqsa ya Oktoba 7, 2023 iliyofanywa na wanamapambano wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS ilifichua namna utawala haramu wa Israel ulivyo dhaifu sanjari na kuugutusha ulimwengu juu ya kadhia ya Palestina.
-
Nigeria kuandamana leo kupinga ongezeko la gharama za maisha
Oct 01, 2024 02:18Wananchi wa Nigeria leo Jumanne wamepanga kufanya maandamano mapya kulalamikia ongezeko la gharama za maisha. Maandamano hayo yaliyopewa jina la "Oktoba Mosi Bila Hofu" yamepangwa kwenda sambamba na kumbukumbu ya maadhimisho ya miaka 64 ya uhuru wa Nigeria.
-
Seneta wa Nigeria: Jinai za Israel Gaza, Lebanon zinaonyesha UN haina maana
Sep 27, 2024 03:05Mwanasiasa wa ngazi ya juu wa Nigeria amesema kuwa, mauaji ya kimbari ya Israel dhidi ya raia wa Palestina katika Ukanda wa Gaza na huko Beirut, mji mkuu wa Lebanon yameonyesha kushindwa kwa dunia kushughulikia suala la Palestina, na pia imeonyesha namna Umoja wa Mataifa ulivyo butu kwa kushindwa kukomesha ukatili na unyama wa Israel.
-
Mafuriko makubwa yaziathiri Nigeria na Niger; mamia ya maelfu ya watu wahama makazi yao
Sep 25, 2024 02:25Mafuriko makubwa yamesababisha maafa katika nchi za kati na magharibi mwa Afrika, zikiwemo Nigeria na Niger na kuathiri mamia ya maelfu ya watu na kusababisha uharibifu mkubwa.