Mlipuko wa kipindupindu wauwa watu 13 katika jimbo la Niger, nchini Nigeria
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i128700-mlipuko_wa_kipindupindu_wauwa_watu_13_katika_jimbo_la_niger_nchini_nigeria
Takriban watu 13 wamefariki dunia na wengine 239 wameambukizwa ugonjwa wa kipindupindu unaoendelea kuenea katika wilaya sita za jimbo la Niger katikati mwa Nigeria. Taarifa hii imetolewa na mamlaka husika katika jimbo la Niger.
(last modified 2025-07-24T10:31:04+00:00 )
Jul 24, 2025 10:31 UTC
  • Mlipuko wa kipindupindu wauwa watu 13 katika jimbo la Niger, nchini Nigeria

Takriban watu 13 wamefariki dunia na wengine 239 wameambukizwa ugonjwa wa kipindupindu unaoendelea kuenea katika wilaya sita za jimbo la Niger katikati mwa Nigeria. Taarifa hii imetolewa na mamlaka husika katika jimbo la Niger.

Ibrahim Ahmed Dangana, Kamishna wa Huduma ya Afya ya Msingi katika Jimbo la Niger amesema katika mkutano na waandishi wa habari kwamba mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu unaendelea kuenea katika maeneo sita ya jimbo hilo. 

Ameongeza kuwa, serikali imeweka vituo vya matibabu na maeneo yaliyotengwa maalumu kwa ajili ya kuwahudumiwa wagonjwa katika kila eneo lililoathiriwa ili kudhibiti ugonjwa huo.

Mlipuko wa kipindupindu unashuhudiwa sasa nchini Nigeria baada ya nchi hiyo kutangaza "dharura ya kitaifa" juu ya ugonjwa huo tarehe 26 mwezi Juni mwaka huu.

Ugonjwa wa kipindupindu unasababishwa na bakteria kwa jina la Vibrio cholerae. Ugonjwa huu huambukiza kupitia chakula na maji machafu. Kipindupindu kinaweza kumsababishia  mgonjwa kupungukiwa pakubwa na maji mwilini na kupoteza maisha ikiwa hatatibiwa.