-
António Guterres: Israel ijiepushe kufanya ukatili huko Quds
Jul 23, 2017 02:14Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameeleza wasiwasi wake kuhusu ukatili na hatua ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kuwazuia Wapalestina kutekeleza ibada ya Swala ndani ya Msikiti wa al Aqsa.
-
Kiongozi wa Kikristo Palestina awataka Wakristo na dunia kuzuia uvamizi wa Wazayuni wa Israel
Jul 19, 2017 09:33Kiongozi wa Kikristo wa kanisa la Orthodox huko Palestina Atallah Hanna, ameomba msaada wa haraka kutoka kwa Wakristo na taasisi za kutetea haki za binaadamu duniani, kuzuia uvamizi wa Wazayuni wa Israel huko Quds.
-
HAMAS: Iran inaendelea kuunga mkono mapambano ya Palestina
Jul 09, 2017 03:09Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaendelea kuunga mkono mapambano ya wananchi wa Palestina na hakuna wakati ambao Tehran ilisitisha himaya na uungaji mkono wake huo.
-
Israel; hatari kuu ya ulimwengu wa Kiislamu
Jun 28, 2017 23:42Naibu Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Waislamu wa Kishia nchini Lebanon amesema kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel ndiyo hatari kuu kwa umma wa Kiislamu na kwamba kitendo cha baadhi ya nchi za Kiislamu cha kuwa na uhusiano na Israel ni hatari kubwa kwa Waislamu.
-
Waislamu kote duniani watakiwa kushiriki kwa wingi Siku ya Kimataifa ya Quds
Jun 20, 2017 03:31Mjumbe wa harakati ya Jihad Islami ya Palestina mjini Tehran ametoa mwito kwa Waislamu kote duniani kushiriki kwa wingi katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds Ijumaa ijayo.
-
Onyo kuhusu Quds na kulegeza kamba Donald Trump
Jun 03, 2017 02:48Walimwengu wamezidi kukasirishwa na ukandamizaji unaoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika mji mtakatifu wa Quds. Huku hayo yakiripotiwa, Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imetoa mwito wa kuitishwa Ijumaa ya ghadhabu dhidi ya utawala wa Kizayuni.
-
Jihadul-Islam, yauonya vikali utawala wa Kizayuni wa Israel
May 16, 2017 03:50Brigedia ya Quds tawi la harakati ya muqawama ya Jihadul-Islami ya Palestina sambamba na kuonyesha picha na video kuhusiana na mwendelezo wa siasa za sasa za utawala huo dhidi ya taifa la Palestina na Ukanda wa Gaza, imetoa indhari kali kwa utawala huo.
-
Wazayuni waendelea kujenga vitongoji vya Wazayuni katika ardhi za Wapalestina
Apr 19, 2017 21:56Licha ya dunia nzima kulalamikia vikali jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel za kupora ardhi za Wapalestina na ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni, lakini viongozi wa Israel wamepasisha mradi wa kujenga nyumba 212 za walowezi wa Kizayuni katika mji unaokaliwa kwa mabavu wa Baytul Muqaddas.
-
Hamas yalaani muswada wa sheria ya Israel wa kuzima adhana Quds
Mar 11, 2017 02:52Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina Hamas imekosoa vikali muswada wa sheria uliopasishwa hivi karibuni na Bunge la utawala wa Kizayuni wa Israel, unaopania kupiga marufuku kusomwa adhana katika misikiti ya Quds tukufu.
-
Haaretz: Balozi mtarajiwa wa Marekani huko Israel amechangia kunyakuliwa ardhi za Wapalestina
Mar 07, 2017 12:04Gazeti la utawala wa Kizayuni wa Israel la Haaretz limefichua kuwa balozi mtarajiwa wa Marekani huko Israel, David Friedman kwa miaka mingi amekuwa akitoa kiwango kikubwa cha fedha kwa ajili ya kunyakua ardhi za Waislamu katika eneo al Quds (Jerusalem) na kuwapa makazi huko Wazayuni.