António Guterres: Israel ijiepushe kufanya ukatili huko Quds
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i32140-antónio_guterres_israel_ijiepushe_kufanya_ukatili_huko_quds
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameeleza wasiwasi wake kuhusu ukatili na hatua ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kuwazuia Wapalestina kutekeleza ibada ya Swala ndani ya Msikiti wa al Aqsa. 
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Jul 23, 2017 02:14 UTC
  • António Guterres: Israel ijiepushe kufanya ukatili huko Quds

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameeleza wasiwasi wake kuhusu ukatili na hatua ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kuwazuia Wapalestina kutekeleza ibada ya Swala ndani ya Msikiti wa al Aqsa. 

António Guterres ameitaka Israel kujiepusha na hatua zote za utumiaji mabavu katika mji unaokaliwa kwa mabavu wa Quds (Jerusalem).

Wiki iliyopita serikali ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu ilifunga milango yote ya kuingia katika Msikiti mtakatifu wa al Aqsa na kuweka kamera na vituo vya upekezi katika maeneo ya kuingilia katika viwanja vya msikiti huo. Hatua hizo zilichukuliwa baada ya mapigano yaliyotokea katika eneo hilo ambapo vijana watatu wa Kipalestina waliuawa shahidi na askari wawili wa Israel waliangamizwa. 

Askari wa Israel wakinyanyasa mwanamke wa Kipalestina, Quds

Viongozi wa nchi nyingi duniani wamelaani hatua ya utawala haramu wa Isarel ya kufunga milango ya kuingia katika Msikiti wa al Aqsa na kuwazuia Waisalmu kufanya ibada. Nchi mbalimbali pia zinaituhumu Israel kwamba imetumia vibaya tukio la kuuliwa askari wake wawili kwa ajili ya kuwazuia Waislamu kufanya ibada katika msikiti huo. 

Wakati huo huo Chuo Kikuu cha al Azhar nchini Miri kimeuonya utawala wa Kizayuni wa Israel kutokana na jinai unazozifanya pambizoni mwa Msikiti wa al Aqsa na kusisitiza kuwa, jinai hizo zinawaumiza Waislamu wote duniani.