-
Russia yataka BRICS iunde mbadala wa IMF
Oct 11, 2024 10:32Russia ambayo ni mwenyekiti wa kiduru wa kundi la BRICS mwaka huu, imetoa wito kwa washirika wake kubuni njia mbadala ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) kukabiliana na shinikizo la kisiasa kutoka mataifa ya magharibi kabla ya mkutano wa kilele wa BRICS baadaye mwezi huu.
-
China na Russia zakosoa jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel
Oct 10, 2024 07:13Wawakilishi wa Kudumu wa China na Russia katika Umoja wa Mataifa wameikosoa vikali Israel kwa kushindwa kutafuta amani na kuzuia juhudi za kukomesha mauaji ya watu wa Palestina.
-
Korea Kusini yadai: Askari wa Korea Kaskazini wanapigana bega kwa bega na Russia Ukraine
Oct 09, 2024 02:25Waziri wa Ulinzi wa Korea Kusini amesema, inavyoonekana wanajeshi wa Korea Kaskazini wanapigana bega kwa bega na wanajeshi wa Russia nchini Ukraine.
-
Putin aamuru mwongozo wa utumiaji silaha za nyuklia wa Russia ufanyiwe mabadiliko
Sep 26, 2024 05:09Rais Vladimir Putin wa Russia ameamuru mwongozo wa utumiaji silaha za nyuklia wa nchi hiyo ufanyiwe mabadiliko akionya pia kuwa nchi yake inaweza kujibu mapigo kwa silaha za nyuklia ikiwa itashambuliwa kwa silaha za kawaida zilizotolewa na dola linalomiliki silaha hizo.
-
Russia: Azimio la Umoja wa Mataifa linaweka wazi uharamu wa vitendo vya Israel
Sep 20, 2024 12:42Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imetangaza kuwa, azimio jipya la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ni hatua muhimu ambayo inaiwezesha jamii ya kimataifa kutambua uharamu wa hatua za Israel.
-
Askari wa Israel waziporomosha kwa mateke maiti za Wapalestina kutokea kwenye paa la jengo
Sep 20, 2024 07:40Askari katili wa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel wamedhihirisha tena unyama wao baada ya kunaswa kupitia mkanda wa video wakiziporomosha kwa mateke maiti za Wapalestina waliowaua katika shambulio walilofanya katika eneo la Qabatiya, Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan unaokaliwa kwa mabavu.
-
Iran: Hatuna nafasi yoyote katika vita vya Russia na Ukraine
Sep 08, 2024 12:04Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu haina mchango wowote katika vita vinavyoendelea kati ya Russia na Ukraine, na daima imekuwa ikikariri wito wake wa mazungumzo ya kuutafutia ufumbuzi mzozo huo.
-
Iran yakanusha madai ya Magharibi: Hatujaipatia Russia makombora yoyote ya balestiki
Sep 07, 2024 11:53Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekanusha madai kwamba inaipatia Russia makombora ya balestiki na kusisitiza kuwa madai hayo yanayotolewa na Marekani na washirika wake wa Magharibi ni ya upotoshaji na hayana msingi wowote.
-
Rais wa Iran kushiriki mkutano wa BRICS nchini Russia
Aug 31, 2024 13:05Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian anatazamiwa kushiriki Mkutano wa BRICS wa 2024 nchini Russia karibuni hivi.
-
Iran yakanusha madai ya kuwapa mafunzo askari wa Russia huko Ukraine
Aug 31, 2024 11:48Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amepuuzilia mbali madai kwamba mwanajeshi wa Jamhuri ya Kiislamu amekuwa akitoa mafunzo kwa wanajeshi wa Russia katika ardhi ya Ukraine.