-
Balozi wa Russia UN: Mashambulizi ya Magharibi dhidi ya Yemen ni kinyume cha sheria
May 15, 2024 02:38Balozi wa Russia katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa mashambulizi ya muungano wa nchi za Magharibi unaoongozwa na Marekani dhidi ya Yemen yamekiuka Mkataba wa Umoja wa Mataifa na hayana uhalali wowote.
-
Askari 1,400 wa Ukraine wauawa Donetsk, Luhansk ndani ya saa 24
May 14, 2024 06:54Wizara ya Ulinzi ya Russia imetangaza habari ya kuuawa wanajeshi 1,400 wa Ukraine katika muda wa saa 24 katika maeneo ya mashariki ya Luhansk na Donetsk, yaliyojitangazia uhuru mwaka 2014, baada ya kutokea mapinduzi nchini Ukraine.
-
Russia yatangaza, imeharibu kambi 2 za magaidi nchini Syria
May 06, 2024 07:12Wizara ya Ulinzi ya Russia imetangaza kuwa imeharibu kambi mbili za magaidi wanaosaidiwa na Marekani huko magharibi mwa Syria.
-
Russia yaruhusu wanawake Waislamu wanaoomba uraia kutumia picha za vazi la Hijabu
May 01, 2024 07:22Serikali ya Russia imelegeza masharti ya kanuni zinazohusu maombi ya raia wa kigeni wanaoomba uraia, na itaruhusu mwanamke wa Kiislamu kutumia picha za paspoti zinazomuonesha akiwa amevaa vazi la staha la Kiislamu la Hijabu. Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo.
-
Waziri wa Ulinzi wa Russia: Ukraine imeshapoteza karibu askari nusu milioni
Apr 23, 2024 23:13Waziri wa Ulinzi wa Russia Sergey Shoigu amesema, hasara za kijeshi ilizopata Ukraine za kuuawa askari wake tangu Februari 2022 hadi sasa zimefikia karibu wanajeshi 500,000.
-
Onyo jipya kuhusu kuingia NATO katika vita vya Ukraine
Apr 23, 2024 00:55Viktor Orbán, Waziri Mkuu wa Hungary amesema katika taarifa kwamba viongozi wa Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Kujihami ya Kijeshi ya Magharibi (NATO) wanauchukulia mzozo wa Moscow na Kyiv kuwa ni wao na wala hawazingatii hatari ya kujihusisha na mzozo huo. Ameonya kuwa NATO inakaribia kutuma askari wake huko Ukraine.
-
Mufti Mkuu wa Russia: Kiongozi Muadhamu wa Iran anastahiki kupongezwa
Apr 21, 2024 23:02Mkuu wa Idara ya Masuala ya Kidini ya Waislamu ya Russia amesema kuwa, mwito unaotolewa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei wa kuwataka watu wote duniani kuthamini masuala ya kidini na kimaadili unastahiki kupongezwa.
-
Russia yakumbwa na mafuriko; nyumba zaidi ya elfu 15 zazama majini
Apr 15, 2024 23:22Maafisa wa Russia wa Idara ya Kukabiliana na Majanga ya Kimaumbile wameeleza kuwa idadi ya nyumba zilizozama kutokana na mafuriko nchini humo imepindukia 15,000.
-
Russia yakosoa kimya cha Baraza la Usalama baada ya shambulio la Israel katika ubalozi mdogo wa Iran, Syria
Apr 15, 2024 00:58Russia imekosoa hatua ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ya kushindwa kuchukua hatua inayofaa baada ya utawala wa Israel kushambulia jengo la ubalozi mdogo wa Iran huko Damascus mji mkuu wa Syria.
-
Russia yataka kutekelezwa haraka amri ya Umoja wa Mataifa ya kukomeshwa vita Ghaza
Apr 11, 2024 06:24Russia imetaka kutekelezwa haraka na bila ya masharti azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu kusimamishwa mara moja mashambulizi ya Israel kwenye Ukanda wa Ghaza.