-
Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi afungua mashindano ya baskeli ya Afrika Mashariki na Kati
Dec 12, 2017 04:49Jumuiya ya Afrika Mashariki imeandaa mashindano ya baskeli nchini Burundi yaliyitishwa kamaishara ya amani nchini humo. Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ambaye pia ni mshiriki wa mashindano hayo ndiye aliyeyazindua. Mwandishi wetu Hamida Issa na maelezo zaidi:
-
Watanzania watakiwa kutojipweteka kuhusu maambukizi ya Ukimwi + Sauti
Dec 01, 2017 14:27Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hasan amewaasa wananchi kutobweteka na kuridhika na hali ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI bali wajali afya zao ili kuweza kufikia lengo la tisini tatu iTapofika mwaka 2020 na kuumaliza kabisa ukimwi nchini Tanzania ifikapo mwaka 2030. Takwimu zinaonesha kuwa Watanzania milioni 1.4 wanaishi na virusi vya UKIMWI. Mwandishi wetu Silvano Kayera kutoka Dar es Salaam Tanzania ana taarifa zaidi.
-
Mazungumzo ya Burundi kuanza Jumanne mjini Arusha Tanzania + Sauti
Nov 27, 2017 14:39Mazungumzo ya kusaka amani nchini Burundi yataanza Jumanne wiki hii mjini Arusha Tanzania chini ya upatanishi wa Rais Mstaafu wa Tanzania Benjamini Mkapa. Hata hivyo kumekuwa na misimamo tafauti huku baadhi wakiunga mkono mazungumzo hayo; na wengine wakisema majadiliano hayo hayana umuhimu. Mwandishi wetu wa Bujumbura Hamida Issa ametutumia ripoti ifuatayo.
-
Bomoabomoa yazikumba ofisi za Tanesco na Wizara ya Maji nchini Tanzania + Sauti
Nov 27, 2017 14:34Zoezi la bomoabomoa katika ofisi za Tanesco na Wizara ya Maji nchini Tanzania zilizopo katika jiji la Dar es Salaam limeanza rasmi ikiwa ni takribani wiki mbili tu zimepita tangu rais John Pombe Magufuli wa nchi hiyo auagize wakala wa barabara nchini humo Tanroads kufanya zoezi hilo. Taarifa zaidi anazo mwandishi wetu Silvano Kayera kutoka Dar es Salaam
-
Waislamu Mombasa Kenya walalamikia mavazi ya nusu uchi + Sauti
Nov 24, 2017 02:41Waislamu nchini Kenya wamekosoa vikali tabia ya baadhi ya vijana kuvaa mavazi yasiyo ya heshima na kutoa mwito kwa serikali ya Kenya kuiga mfano wa Uganda ambayo inashinikiza mavazi ya heshima hasa katika maeneo ya umma. Seifullah Murtadha na maelezo zaidi
-
Rwanda kupokea maelfu ya wahamiaji waliokwama Libya + Sauti
Nov 24, 2017 02:36Serikali ya Rwanda imesema kuwa iko tayari kupokea wahamiaji zaidi ya 30,000 wa Kiafrika waliokwama nchini Libya na ambao wanapigwa mnada sokoni na kuuzwa kama bidhaa.
-
Salum Bendera na ripoti ya kumbukumbu za Arubaini ya Imam Husain AS, Karbala Iraq
Nov 11, 2017 07:42Jana Ijumaa mwezi 20 Mfunguo Tano Safar sawa na tarehe 10 Novemba 2017 ilisadifiana na Arubaini ya Imam Husain AS kwa mujibu wa kalenda ya Iraq. Mamilioni ya Waislamu kutoka kona mbalimbali za dunia wameshiriki katika kumbukumbu hizo zilizofikia kileleni jana huko Karbala Iraq. Mwenzetu Salumu Bendedra aliyetumwa maalumu kuakisi tukio hilo ametutayarishia ripoti ifuatayo
-
Mahojino na Sheikh Ghauth Nyambwa akiwa Karbala Iraq
Nov 11, 2017 07:35Kumbukumbu za Arubaini ya Imam Husain ambazo hufikia kileleni mwezi 20 Mfunguo Tano Safar kila mwaka huko Karbala Iraq, zinawajumuisha pamoja mamilioni ya wapenzi wa Ahlul Bayt AS kutoka kona zote za dunia.
-
Uonevu dhidi ya waandishi wa habari
Nov 03, 2017 05:44Baraza la habari Tanzania limepanga kuwapeleka mahakamani wale wanaotishia na kufanya uhalifu kwa wanahabari kwani ni jambo ambalo linaleta hofu kwao na kupelekea washindwe kufanya kazi kwa ufanisi Mwandishi wetu Silvano Kayera kutoka Dar es Salaam Tanzania anataarifa zaidi.
-
Kuendelea tafiti za kusaka Katiba Mpya nchini Tanzania + SAUTI
Oct 19, 2017 12:51Wananchi wa Tanzania wameendelea kuunga mkono kwa nguvu kubwa uundwaji wa katiba mpya inayotilia mkazo suala la uwajibikaji huku asilimia 79 wanataka mawaziri wanaoteuliwa wapitishwe na bunge na asilimia 64 wanataka wawe na uwezo wa kuwaondoa wabunge katikati ya uchaguzi iwapo hawatatekeleza majukumu yao ipasavyo Mwandishi wetu Silvano Kayera kutoka dar es salaam Tanzania ana taarifa zaidi…