-
Umuhimu wa Vyuo Vikuu vya Afrika kuwa na mtaala mmoja wa masomo + SAUTI
Oct 19, 2017 12:40Vyuo vikuu vya mataifa ya kusini mwa jangwa la Sahara vimetangaza kuwa viko tayari kutengeneza mitaala inayoendana na mahitaji ya jamii ya wakazi wa bara la Afrika. Watalaamu kutoka vyuo vikuu vya mataifa ya kusini mwa jangwa hilo wamesema, kanda hiyo inaendelea kuwa na matatizo ya maendeleo duni kutokana na wahitimu wa vyuo vikuu kutokuwa na uwezo wa kutatua matatizo yanayozikabili jamii zao. Kutoka Kigali mwandishi wetu Sylvanus Karemera anaripoti zaidi
-
SAUTI: Waandishi Burundi walalamikia wanavyobanwa, mazingira hatari na ukosefu wa usalama kazini
May 04, 2017 13:34Mkuu wa kituo cha waandishi habari nchini Burundi amesema, maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari yanafanyika wakati waandishi nchini humo wakifanya kazi katika hali ya woga kiasi kwamba katika kipindi cha miaka miwili ya mzozo wa nchi hiyo uhuru wa vyombo vya habari umebakia katika maandishi na si katika vitendo. Maelezo zaidi na mwandishi wa Bujumbura, Hamida Issa...
-
SAUTI: Radio Tehran yahojiana na wakimbizi wa Rwanda mjini Brazzaville
Apr 11, 2017 02:38Wakimbizi kutoka Rwanda wanaoishi nchini Kongo Brazzaville wamefanya maombi ya kumbukumbu ya mauaji ya kimbari yaliyojiri nchini mwao mwaka 1994. Mwandishi wa Radio Tehran aliyeko mjini Brazzaville amefanya mahojiano maalumu na mwakilishi wa wakimbizi hao...
-
SAUTI: Makumi ya shule zina hatari ya kufungwa Burundi
Apr 11, 2017 02:27Wizara ya Elimu nchini Burundi imetoa tahadhari ya kuzifunga shule 40 nchini humo kutokana na kupata alama ya chini ya asiimia 20 katika mitihani ya kuingia sekondari. Mwandishi wa Radio Tehran na ripoti kamili kutoka Bujumbura...
-
SAUTI: Mgomo walemaza harakati za kijamii DRC
Apr 04, 2017 05:52Miji mikubwa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeripotiwa kupooza kufuatia mgomo ulioitishwa na wapinzani wanaoishinikiza serikali isaidi mkataba wa amani uliofikiwa tarehe 31 Disemba mwaka jana. Mossi Mwasi ana maelezo zaidi kutoka Congo Brazzaville.
-
SAUTI: Hali mbaya ya usalama nchini Uganda
Apr 04, 2017 05:37Vitisho vipya dhidi ya usalama wa Uganda hususan usalama wa jeshi la polisi vimejitokeza nchini humo hivi sasa uchunguzi ukiendelea kufanyika kuhusiana na suala hilo. Mwandishi wetu Kigozi Ismail amettumia ripoti ifuatayo:
-
SAUTI: Serikali Burundi yatumai wakimbizi watarejea; wakimbizi lakini hawaoneshi hamu wa kurejea nyumbani
Feb 19, 2017 10:46Viongozi wa Burundi wameonesha matumaini makubwa ya kurejea nyumbani raia wa nchi hiyo waliokomimbilia nchi jirani baada ya kazuka machafuko nchi mwao hasa baada ya chama tawala cha CNDD-FDD kumuidhinisha Rais Pierre Nkurunziza kugombea urais kwa mara ya tatu mfululizo. Maelezo zaidi anayo mwandishi wa wetu wa Kampala, Uganda, Kigozi Ismail.
-
SAUTI: Kiswahili lugha rasmi nchini Rwanda, Kifaransa chatupwa
Feb 13, 2017 12:13Wananchi wa Rwanda wamefurahishwa na uamuzi wa bunge la nchi hiyo wa kupitisha Kiswahili kama lugha rasmi nchini humo.
-
SAUTI: Vita dhidi ya mihadarati nchini Tanzania
Feb 05, 2017 03:37Jeshi la Polisi nchini Tanzania pamoja na serikali ya nchi hiyo imetupiwa lawama za kukithiri biashara haramu ya dawa za kulevya na kuongezeka idadi ya watumiaji wa dawa hizo haramu. Mwandishi wa Radio Tehran wa jijini Dar es Salaam Tanzania, amefuatilia jambo hilo na kutuandalia ripoti ifuatayo.
-
SAUTI: Mahojiano na Naibu Mufti wa Malawi kuhusu Umoja wa Waislamu
Dec 20, 2016 07:27Mkutano wa 30 wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu ulimalizika Jumamosi usiku mjini Tehran kwa taarifa iliyosisitiza ulazima wa kuwepo mshikamano katika ulimwengu wa Kiislamu na kuchukuliwa tahadhari dhidi ya njama za maadui za kuibua mifarakano katika nchi za Kiislamu.