SAUTI: Mahojiano na Naibu Mufti wa Malawi kuhusu Umoja wa Waislamu
Mkutano wa 30 wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu ulimalizika Jumamosi usiku mjini Tehran kwa taarifa iliyosisitiza ulazima wa kuwepo mshikamano katika ulimwengu wa Kiislamu na kuchukuliwa tahadhari dhidi ya njama za maadui za kuibua mifarakano katika nchi za Kiislamu.
Taarifa hiyo ya mwisho ilikuwa na vipengee 27 ambapo washiriki wa mkutano huo wa siku tatu walichunguza matukio ya hivi karibuni katika nchi za Kiislamu. Aidha walijadili udharura wa kuwepo mipango ya kuondoa hitilafu zilizopo katika Ulimwengu wa Kiislamu. Taarifa hiyo imeongeza kuwa kuna udharura wa kuimarisha umoja wa Kiislamu ili kukabiliana na wimbi la wakufurishaji ambao wanaeneza fikra zilizo dhidi ya Umoja wa Kiislamu.
Mkutano wa 30 wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu ulianza Alhamisi kwa kauli mbiu ya 'Umoja na Udharura wa Kukabiliana na Makundi ya Wakufurishaji.' Mkutano huo ulihudhuriwa na wasomi na wanasiasa kutoka nchi zaidi ya 60 duniani. Kati ya waliohudhuria mkutano huo kutoka barani Afrika ni Sheikh Shuaib Ibrahim, Naibu Mufti wa Malawi ambaye alizungumza na Amir Ibrahim wa Radio Tehran na hapa ameanza kutoa tathmini yake kuhusu mkutano huo.