Rwanda kupokea maelfu ya wahamiaji waliokwama Libya + Sauti
Nov 24, 2017 02:36 UTC
Serikali ya Rwanda imesema kuwa iko tayari kupokea wahamiaji zaidi ya 30,000 wa Kiafrika waliokwama nchini Libya na ambao wanapigwa mnada sokoni na kuuzwa kama bidhaa.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Bi Louise Mushikiwabo amesema, ijapokuwa Rwanda haina eneo kubwa la ardhi lakini haiwezi kuwaacha Waafrika wenzao wakiendelea kufanyiwa vitendo vya kinyama na vya aibu kama hivyo. Mwandishi wa Radio Tehran Sylvanus Karemera na ripoti zaidi kutoka Kigali.
Tags