Kundi la kigaidi linaloaminika kuwa na mfungamano na al-Shabaab ya Somalia limevamia kijiji kimoja katika mkoa wa Cabo Delgado kaskazini mwa Msumbiji na kuua watu saba kwa kuwakata vichwa.
Kwa akali watu saba wameuawa katika shambulizi la kigaidi lililotokea karibu na msikiti mmoja kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Mashambulizi matatu ya kigaidi dhidi ya makanisa yamepelekea watu wasiopungua 10 kuuawa na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa nchini Indonesia.
Kwa akali watu 14 wameuawa baada ya kundi la kigaidi kushambulia kwa mabomu na risasi makao makuu ya Tume ya Uchaguzi nchini Libya leo Jumatano.
Mashambulizi pacha ya mabomu yameua waumini watatu wa Kiislamu msikitini katika mji wa Bama jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani shambulio la kigaidi lililotekelezwa leo huko Kabul mji mkuu wa Afghanistan na kulitaja kuwa ni kitendo cha jinai na kisicho cha kibinadamu.
Kwa akali watu sita wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia milipuko pacha ya mabomu iliyotokea katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu jana Ijumaa.
Makumi ya watu wameripotiwa kupoteza maisha katika shambulizi la bomu la kutegwa ardhini linaloaminika kufanywa na kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh (ISIS) nchini Mali.
Watu 12 wameuawa na makumi ya wengine wamejeruhiwa katika shambulio la kujilipua kwa bomu lililotekelezwa sokoni katika jimbo la Borno kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Kundi la kigaidi na kitakfiri la al-Shabaab linadai kwamba limeua askari watano wa Kikosi cha Askari wa Kulinda Amani cha Umoja wa Afrika Amisom katika mlipuko wa bomu uliotokea mjini Mogadishu jana Jumapili.