Kwa akali watu 40 wameuwa na wengine 30 kujeruhiwa katika shambulizi la kigaidi lililoutikisa mji mkuu wa Afghanistan, Kabul.
Mshambuliaji aliyekuwa amejifunga bomu amejiripua na kuua watu wawili katika msikiti mmoja ulioko kaskazini mwa Cameroon karibu na mpaka wa nchi hiyo na Nigeria mapema leo.
Kwa akali watu watatu wamejeruhiwa katika shambulizi la guruneti nchini Burkina Faso, lililofanyika masaa machache kabla ya Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa kuanza ziara ya kuitembelea nchi hiyo ya Kiafrika.
Viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wameendelea kulaani vikali shambulizi la kigaidi lililolenga Waislamu waliokuwa wakitekeleza ibada ya Swala ya Ijumaa msikitini katika eneo la Sinai nchini Misri na kuua mamia ya watu wasio na hatia yoyote.
Kwa akali watu 185 wameuawa na makumi ya wengine wamejeruhiwa katika shambulizi la kigaidi dhidi ya msikiti mmoja katika Peninsula ya Sinai nchini Misri.
Watu wasiopungua 50 wameaga dunia katika mlipuko wa bomu uliotokea msikitini kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Kwa akali watu 50 wameuawa katika shambulio la bomu dhidi ya msikiti mmoja ulioko kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Kwa akali watu 10 wameuawa katika shambulizi la kundi la kigaidi lenye mafungamano la genge la kitakfiri la Daesh (ISIS) katika eneo la Sinai nchini Misri.
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Marekani inafanya juu chini kupotosha ukweli wa mambo kuhusu mashambulio ya kigaidi ya Septemba 11 mwaka 2001.
Wakuu wa vyombo vya usalama nchini Somalia wamepigwa kalamu nyekundu kufuatia mashambulizi ya kigaidi ya jana Jumamosi yaliyosababisha makumi ya watu kuuawa na kujeruhiwa.