-
Yemen: Saudia na washirika wake wanatumia silaha za Marekani, Uingereza na Ufaransa dhidi ya raia
Jan 19, 2020 13:21Waziri Mkuu wa Serikali ya Uokovu ya Yemen amesema kuwa, muungano unaoongozwa na Saudi Arabia unatumia silaha hatari zilizotengenezwa na Marekani, Uingireza na Ufaransa dhidi ya raia wa Yemen.
-
Kushtakiwa Ujerumani katika Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu (ICJ) kwa kuiuzia silaha Saudia
Dec 19, 2019 02:31Kuendelea vita vya Yemen na kuuawa maelfu ya raia wa nchi hiyo katika vita hivyo, kumezipelekea baadhi ya asasi na mashirika ya haki za binaadamu kukosoa vikali siasa mbovu na hatua za nchi za Ulaya ikiwemo ya kuuzia silaha muungano vamizi wa Saudia unaoongoza vita hivyo dhidi ya Yemen.
-
Ijumaa Nyeusi, Wamarekani walinunua silaha zinazolitosha jeshi la nchi kavu
Dec 04, 2019 03:01Idara ya Upepezi ya Marekani (FBI) imetangaza kwamba imepokea maombi zaidi ya laki mbili ya kufanya uchunguzi kuhusiana na mauzo ya silaha za moto kwa mnasaba wa siku ya Ijumaa Nyeusi (Black Friday), kiwango ambacho ni cha pili kwa ukubwa cha mauzo ya silaha tangu mwaka 1998.
-
Afrika Kusini yasitisha uuzaji silaha kwa Saudia, UAE
Nov 23, 2019 11:57Afrika Kusini imetangaza kuwa inasitisha uuzaji wa silaha zake kwa Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) baada ya kubainika kuwa tawala hizo mbili zinawakabidhi wanamgambo wa Yemen baadhi ya silaha hizo na hivyo kukiuka mapatano ambayo yanazuia silaha zilizonunuliwa kutoka Afrika Kusini kufikia pande za tatu.
-
Vyombo vya habari vyafichua, Marekani inapeleka silaha kwa siri huko Yemen
Nov 08, 2019 14:28Vyombo vya habari vimefichua kwamba, wiki iliyopita zana na silaha za kivita za Marekani ziliingizwa kusini mwa Yemen zikibebwa na meli ya Saudi Arabia.
-
Kuuziwa silaha Saudi Arabia; mwendelezo wa siasa za kindumakuwili za madola ya Ulaya mkabala na vita vya Yemen
Oct 11, 2019 12:21Katika hali ambayo, muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia ungali unaendelea kufanya mauaji huko nchini Yemen, na madola ya Magharibi nayo yameendelea kuiimarisha kijeshi Riyadh kutokana na kuipatia silaha na zana za kijeshi, Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amejitoa kimasomaso na kuzitaka Saudia na Imarati kutotumia katika vita vyao huko Yemen silaha zilizotengenezwa nchini Ufaransa kwani kufanya hivyo kunaweza kupelekea kuuawa raia.
-
Papa azikosoa nchi zinazouza silaha na kuwafukuza wakimbizi
Sep 30, 2019 07:45Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amesema mashindano ya kuuza silaha yanayofanywa na nchi fulani duniani ndiyo sababu ya ghasia na mauaji ya watu wakiwemo watoto wadogo katika nchi zinazoshuhudia vita katika kona mbalimbali duniani.
-
Uingereza yakiuka marufuku ya kuiuzia silaha Saudia
Sep 18, 2019 02:39Serikali ya Uingereza imekiri kuwa ilikiuka marufuku ya kuuzia silaha utawala wa Aal-Saud wa Saudi Arabia unaoua raia wasio na hatia huko Yemen.
-
Wapinzani wa vita Uingereza: Serikali ya London inaziunga mkono tawala za kidikteta
Aug 01, 2019 02:55Wanaharakati wanaopinga vita nchini Uingereza (Anti-war Movement) wametangaza kuwa, takwimu za mauzo ya silaha ya nchi hiyo zinaonesha kuwa, London inazizatiti kwa silaha tawala kandamizi na kuziunga mkono.
-
China: Marekani isicheze na moto katika kadhia ya Taiwan
Jul 12, 2019 15:38Waziri wa Mambo ya Nje wa China ameionya vikali Marekani isijaribu kucheza na moto kuhusiana na suala la Taiwan, huku akikosoa vikali mpango wa Washington wa kukiuzia silaha kisiwa hicho ambacho Beijing inasisitiza kuwa ni milki yake.