Ijumaa Nyeusi, Wamarekani walinunua silaha zinazolitosha jeshi la nchi kavu
Idara ya Upepezi ya Marekani (FBI) imetangaza kwamba imepokea maombi zaidi ya laki mbili ya kufanya uchunguzi kuhusiana na mauzo ya silaha za moto kwa mnasaba wa siku ya Ijumaa Nyeusi (Black Friday), kiwango ambacho ni cha pili kwa ukubwa cha mauzo ya silaha tangu mwaka 1998.
Ripoti zinasema kuwa, uuzaji silaha kwa raia nchini Marekani umeogezeka kwa asilimia 11 mwaka huu ikilinganishwa na ule wa Black Friday ya mwaka uliopita.
Vyombo vya habari vya Marekani vinasema kuwa, takwimu hizo haziakisi idadi kamili ya silaha zilizouzwa kwa raia mwaka huu. Takwimu zinaonesha kuwa Wamarekani mwaka huu wamenunua silaha zinazotosha kugawanywa kwa wanajeswhi wote wa kikosi cha nchi kavu cha nchi hiyo wanaokadiriwa kufikia laki moja na elfu 82.
Maelfu ya Wamarekani huuawa kila mwaka katika visa vya kufyatuliana risasi katika maeneo ya umma, mashuleni na kadhalika.
Septemba mwaka jana maafisa karibu 150 wa Baraza la Seneti la Marekani walitoa wito wa kuwekwa sheria kali zaidi za kudhibiti silaha na udhibiti wa watumiaji wa silaha hizo.