-
Mripuko katika mji mkuu wa Somalia waua watu wanane na kujeruhi wengine 10
Nov 26, 2018 12:17Jeshi la polisi nchini Somalia limetangaza habari ya kuuawa na kujeruhiwa watu wasiopungua 18 baada ya gari lililokuwa limetegwa mabomu kuripuka mjini Mogadishu leo Jumatatu.
-
Magaidi wa Al Shabab waua watu 10 katika hujuma mpya Somalia
Nov 26, 2018 04:43Magaidi wakufurishaji wa kundi la Al Shabab nchini Somalia wameshambulia kituo kimoja cha mafunzo ya Kiislamu kati mwa nchi hiyo na kumuua mhubiri na watu wengine tisa waliokuwa hapo.
-
Hujuma ya anga ya Marekani yaua 37 nchini Somalia
Nov 21, 2018 04:16Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) na Kamandi ya Jeshi la Marekani barani Afrika (AFRICOM) zimedai kuwa mashambulizi ya anga ya wanajeshi wake yamefanikiwa kuangamiza wanachama 37 wa kundi la kigaidi na kitakfiri la al-Shabaab nchini Somalia.
-
UN: Waliotekeleza hujuma ya kigaidi Somalia wawajibishwe
Nov 12, 2018 11:50Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani vikali shambulio la kigaidi la Novemba 9 mjini Mogadishu nchini Somalia ambalo limeua raia wengi wasio na hatia na kujeruhi makumi ya wengine.
-
Utafiti: Mashambulizi ya anga ya Marekani huko Somalia hayana tija
Nov 11, 2018 10:50Utafiti mpya umesema mashambulizi ya anga yanayofanywa kila uchao na Marekani nchini Somalia yameshindwa kulitokomeza au hata kulidhoofisha kundi la kigaidi na kitakfiri la al-Shabaab na badala yake yamekuwa na taathira hasi kwa raia wa kawaida.
-
Watu zaidi ya 30 wauawa katika mashambulizi ya kigaidi Mogadishu
Nov 09, 2018 23:56Watu zaidi ya 30 wameuawa katika mashambulizi ya kigaidi yaliyolenga Hoteli ya Sahafi mjini Mogadishu ambayo hutumiwa zaidi na maafisa wa serikali ya Somalia.
-
Mbunge auawa katika mripuko wa bomu Mogadishu, Somalia
Nov 08, 2018 12:18Polisi ya Somalia imesema mbunge mmoja wa eneo la HirShabelle amepoteza maisha katika mripuko wa bomu uliotokea adhuhuri ya leo katika mji mkuu wa nchi hiyo, Mogadishu.
-
Mkuu wa fedha wa al-Shabaab ya Somalia auawa
Oct 26, 2018 10:32Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM kimetangaza habari ya kufanikiwa kumuangamiza Mdhibiti Mkuu wa Fedha wa kundi la kigaidi na ukufurishaji la al-Shabaab.
-
Watu zaidi ya 50 wauawa katika mapigano baina ya koo huko Somaliland, Somalia
Oct 24, 2018 13:01Mapigano yaliyojiri kati ya koo hasimu katika kijiji cha Dhumey eneo la Somaliland lililojitenga na Somalia yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 50.
-
Idadi ya vifo katika miripuko wa Somalia yaongezeka
Oct 15, 2018 04:21Idadi ya wahanga wa mashambulio mawili ya kujiripua kwa mabomu iliyotokea kusini magharibi mwa Somalia imeongezeka. Taarifa zinasema kuwa watu 20 wamepoteza maisha na wengine 40 wamejeruhiwa katika miripuko hiyo miwili iliyopishana kwa dakika chache tu.