-
Sisitizo la Syria la kutokuwa na silaha za kemikali
Sep 10, 2017 06:22Katika kujibu madai ya kamisheni ya uchunguzi inayosimamiwa na Baraza la Haki za Binaadamu la Umoja wa Mataifa, kuhusiana na utumiwaji wa silaha hizo na serikali ya Syria, Damascus imetangaza kuwa haina silaha za namna hiyo.
-
Makumi ya magaidi wa Daesh waangamizwa Deir ez Zor Syria
Sep 08, 2017 14:23Wizara ya Ulinzi ya Russia imetangaza kuwa makumi ya magaidi ya kundi la Daesh wameuawa katika shambulio la ndege za kivita za nchi hiyo katika eneo la Deir ez Zor mashariki mwa Syria.
-
Hamas yalaani shambulizi la anga la Israel nchini Syria
Sep 07, 2017 23:57Harakati ya Mapambnao ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imelaani shambulio la Alkhamisi asubuhi la ndege za utawala wa Kizayuni wa Israel nchini Syria.
-
UN yawataka wapinzani Syria kusalimu amri na kukubali kushindwa
Sep 07, 2017 09:46Mwakilishi Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika Masuala ya Syria ameyataka makundi ya wapinzani katika nchi hiyo ya Kiarabu wasalimu amri na kutangaza kuwa yameshindwa katika mapambano yao ya kuiong'oa madarakani serikali ya Rais Bashar al-Assad.
-
Hezbollah: Kundi la kigaidi la ISIS (Daesh) lilianzishwa na Marekani
Sep 07, 2017 03:22Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon Sheikh Naeem Qassim amesema kundi la kigaidi la ISIS au Daesh liliundwa na Marekani kwa lengo la kutumiwa kuiangusha serikali halali ya Syria inayoongozwa na Rais Bashar al Assad.
-
Kuvunjwa mzingiro wa Deir ez Zor, mwanzo wa kukombolewa Syria yote
Sep 06, 2017 23:50Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imekutaja kuvunjwa mzingiro wa Deir ez Zor huko Syria kuwa ni mwanzo wa kukombolewa maeneo mengine yanayoshikiliwa na kundi la Daesh.
-
Syria yamiminiwa pongezi kwa ushindi wa kistratajia dhidi ya ISIS, Deir ez-Zor
Sep 06, 2017 02:44Duru mbali mbali za kieneo na kimataifa zimeendelea kuipongeza serikali ya Syria baada ya wanajeshi wake kufanikiwa kufika katika mji wa Deir ez-Zor na kuvunja mzingiro wa miaka mitatu uliokuwa umewekwa na kundi la kigaidi la Dash (ISIS).
-
Kamanda wa jeshi la Syria, asema Iran, Syria na Hizbullah hazitashindwa kufelisha njama za adui
Sep 06, 2017 00:00Kamanda wa kikosi cha 104 cha gadi ya rais wa Syria amesema kuwa, harakati ya muqawama inayoundwa na Iran, Syria na Hizullah ya Lebanon, kamwe haitoshindwa, bali pande zote zilizokula njama dhidi ya Syria ndizo zitashindwa na kufeli.
-
Jeshi la Syria lavunja mzingiro wa ISIS Deir ez-Zor
Sep 05, 2017 09:32Jeshi la Syria, likipata himaya ya wapiganaji waitifaki, limefanikiwa kufika katika mji wa Deir ez-Zor na kuvunja mzingiro wa miaka mitatu uliokuwa umewekwa na kundi la kigaidi la ISIS katika mji huo.
-
Hizbullah: Tutaendelea kuweko Syria hadi hatari ya magaidi itakapoondoka
Sep 04, 2017 22:05Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, harakati hiyo ya mapambano ya Kiislamu ambayo iko Syria kwa ombi la serikali ya nchi hiyo, itabakia nchini humo hadi pale hatari ya ugaidi itakapoondoka.