Hezbollah: Kundi la kigaidi la ISIS (Daesh) lilianzishwa na Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i34023-hezbollah_kundi_la_kigaidi_la_isis_(daesh)_lilianzishwa_na_marekani
Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon Sheikh Naeem Qassim amesema kundi la kigaidi la ISIS au Daesh liliundwa na Marekani kwa lengo la kutumiwa kuiangusha serikali halali ya Syria inayoongozwa na Rais Bashar al Assad.
(last modified 2026-03-27T07:58:19+00:00 )
Sep 07, 2017 03:22 UTC
  • Hezbollah: Kundi la kigaidi la ISIS (Daesh) lilianzishwa na Marekani

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon Sheikh Naeem Qassim amesema kundi la kigaidi la ISIS au Daesh liliundwa na Marekani kwa lengo la kutumiwa kuiangusha serikali halali ya Syria inayoongozwa na Rais Bashar al Assad.

Katika mahojiano na Televisheni ya RT, Sheikh Naeem Qassim amesema sera za Marekani nchini Syria na Asia Magharibi kwa ujumla zimefeli na kugonga mwamba.  Amesema: "Marekani ilikuwa inataka kutumia ISIS kufikia malengo yake ya kisiasa, lakini kundi hilo la kigaidi sasa ni tishio kwa Marekani yenyewe."

Kiongozi huyo wa ngazi za juu wa Hizbullah amesema Rais Assad wa Syria ni kiongozi mwenye taathira katika nchi yake na ameiongoza nchi hiyo kwa njia sahihi katika kipindi cha vita. Sheikh Qassim ameendelea kusema kuwa: "Marekani ilikuwa inatamani kuiona Syria ikibadilisha sera zake za kimapambano na kuunga mkono maslahi ya utawala wa Kizayuni wa Israel lakini haikufanikiwa katika hilo."

Magaidi wa ISIS kabla ya kutimuliwa mjini Aleppo nchini Syria

Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema ushirikiano mzuri kati ya Syria, Russia, Iran na Hizbullah ya Lebanon ni jambo ambalo limepelekea maeneo mengi ya Syria yakombolewe kutoka mikononi mwa makundi ya kigaidi.

Mgogoro wa Syria ulianza mwaka 2011 baada ya magaidi kuvamia nchi hiyo  kwa msaada wa Saudi Arabia, Marekani na waitiafake wao wengine katika eneo kama vile Uturuki kwa maslahi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Katika miezi ya hivi karibuni, vikosi vya jeshi la  Syria kwa msaada wa waitifaki limefanikiwa kutoa pigo kubwa kwa magaidi katika maeneo mbali mbali nya nchi hiyo.