-
Waislamu Tanzania wajiandaa kufanya Maulidi ya Mtume Muhammad SAW kwa hamasa kubwa zaidi mwaka huu + Sauti
Oct 07, 2019 06:03Viongozi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) wametoa ufafanuzi kuhusu maandalizi ya Maulidi ya Kitaifa yanavyoendelea jijini Mwanza na wamejipanga kufanya shughuli mbalimbali za kijamii kuelekea maadhimisho hayo ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad SAW. Ammar Dachi na taarifa zaidi kutoka Dar es Salaam...
-
Marais wa Tanzania na Zambia wafungua kituo muhimu cha mpakani
Oct 05, 2019 10:36Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania na mwenzake Edgar Lungu wa Zambia leo Jumamosi wamefungua kituo muhimu cha huduma za pamoja katika mpaka wa nchi hizo mbili kilichoko Tunduma upande wa Tanzania na Nakonde upande Zambia.
-
Wakili wa mwandishi Kabendera amuomba Rais wa Tanzania amsamehe mteja wake
Oct 02, 2019 00:45Wakili wa Erick Kabendera, mwandishi hodari wa habari nchini Tanzania aliyetiwa nguvuni zaidi ya miezi miwili iliyopita, amemwomba rais wa nchi hiyo John Magufuli atoe msamaha kwa mteja wake, wakati mahakama ikiakhirisha kwa mara ya sita kusikilizwa kesi ya mwandishi huyo.
-
IGP Simon Sirro: Jeshi la polisi Tanzania linasumbuliwa na unafiki
Sep 24, 2019 09:37Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania, Inspekta Jenerali, Simon Sirro amesema kuwa tatizo linalolisumbua jeshi hilo ni unafiki.
-
Fatma Karume: Hatuwezi kuishi kwenye nchi iliyo na dhuluma kiasi hiki
Sep 22, 2019 10:16Fatma Karume, wakili wa Tanzania aliyevuliwa uwakili na mahkama ya nchi hiyo amesema kuwa hatokata tamaa na kwamba anatafakari kuingia kwenye siasa kwa lengo la kupigania mabadiliko muhimu nchini na kuhakikisha Watanzania wanaheshimiwa na kuzingatiwa misingi ya demokrasia.
-
Edward Lowassa: Tanzania imewaka moto kila sehemu kutokana na utendaji wa Magufuli
Sep 20, 2019 10:30Waziri Mkuu wa Zamani wa Tanzania, Edward Lowassa amepongeza utendaji kazi wa Rais John Pombe Magufuli wa nchi hiyo kuwa, umeliwasha moto kila mahali taifa hilo.
-
Membe ahimiza uhuru wa vyombo vya habari Tanzania + Sauti
Sep 19, 2019 14:01Aliyekuwa waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki nchini Tanzania Benard Membe amesema kuwa serikali inaweza kuwa dumavu endapo haitoruhusu uhuru wa vyombo vya habari. Amari Dachi na maelezo zaidi kutoka Dar es Salaam Tanzania
-
Watanzania: Wamarekani ndio waliotengeneza Ebola kuwamaliza Waafrika + Sauti
Sep 15, 2019 12:14Kufuatia uvumi wa kuibuka maradhi ya Ebola nchini Tanzania, Watanzania wengi wamekua wakieneza taarifa kwenye mitandao ya kijamii zinazoeleza kuwa, ugonjwa huo ulitengenezwa na Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) kwa lengo la kupunguza idadi ya Waafrika. Tumtegee sikio mwandishi wetu wa Dar es Salaam kwa taarifa kamili...
-
Serikali ya Tanzania: Hakuna ugonjwa wa Ebola nchini
Sep 14, 2019 09:48Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa taarifa ikisema kuwa, hakuna mtu aliyethibitika kuwa na ugonjwa wa Ebola ndani ya nchini hiyo, na kuongeza kwamba, watu wawili waliotiliwa shaka na baadaye kupimwa imethibitika kuwa hawana maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo.
-
Serikali ya Tanzania: Umasikini umepungua sana nchini
Sep 11, 2019 07:58Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imesema kuwa umasikini nchini umepungua kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na miaka ya huko nyuma.