IGP Simon Sirro: Jeshi la polisi Tanzania linasumbuliwa na unafiki
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i56216-igp_simon_sirro_jeshi_la_polisi_tanzania_linasumbuliwa_na_unafiki
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania, Inspekta Jenerali, Simon Sirro amesema kuwa tatizo linalolisumbua jeshi hilo ni unafiki.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 24, 2019 09:37 UTC
  • Inspekta Jenerali, Simon Sirro
    Inspekta Jenerali, Simon Sirro

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania, Inspekta Jenerali, Simon Sirro amesema kuwa tatizo linalolisumbua jeshi hilo ni unafiki.

IGP Sirro ametoa kauli hiyo leo katika ufunguzi wa kikao cha maafisa waandamizi wa polisi kinachofanyika jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa, mwenye wadhifa kama wake nchini Tanzania yupo mmoja tu. "Tatizo linalotusumbua sisi jeshi la polisi ni unafiki. "There is no way tukawa na IGP zaidi ya mmoja, mimi sikujichagua", amesema Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania. Kadhalika (IGP), Simon Sirro amewataka askari polisi kuongeza umakini katika utendajikazi wao kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa akikumbushia vifo vya Akwilina Akwiline, aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) na Daudi Mwangosi, mwandishi wa habari wa kituo cha Channel Ten aliyeuawa Septemba 2, 2012 wakati akiwa kazini.

Akwilina Akwiline, aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT)

Kadhalika kiongozi huyo wa Jeshi la Polisi Tanzania amelitaka jeshi hilo kujiimarisha zaidi hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi huo na kuhakikisha unafanyika katika mazingira salama. 

Sirro aliyeteuliwa tarehe 28 Mei 2017 kuchukua nafasi ya mtangulizi wake, Ernest Mangu amebainisha kwamba, anatamani kumaliza nafasi yangu, huku jeshi la polisi likiwa na heshima yake.